VIJANA WANAOKOSA SIFA ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO WAJIUNGE NA VYUO VYA UFUNDI-DKT.JAFO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 10, 2022

VIJANA WANAOKOSA SIFA ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO WAJIUNGE NA VYUO VYA UFUNDI-DKT.JAFO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Dkt.Seleman Jafo (katikati) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (kushoto) pamoja na Mkuu mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati wa kufungua maonesho ya Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) yanayoendelea jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Dkt.Seleman Jafo (Wa kwanza kulia) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (wa pili kulia) wakiwa wametembelea moja ya mabanda yaliyopo katika maonesho hayo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Dkt.Seleman Jafo (katikati) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (kushoto)  wakiwa wametembelea moja ya mabanda yaliyopo katika maonesho hayo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Dkt.Seleman Jafo (Wa kwanza kulia) sambamba na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (wa pili kulia) wakiwa wametembelea moja ya mabanda yaliyopo katika maonesho hayo

Na Okuly Julius Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na Muungano Seleman Jafo amewataka vijana wanaomaliza elimuya kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kujiunga na vyuo vya kati na ufundi.

WaziriJafo aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya Elimu ya Sayansi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET).

Waziri Jafo amesema takwimu za mwaka jana zinaeleza kuwa wanafunzi 173000 walimaliza kidato cha nne kati yao wanafunzi 90,000 waliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

“Leo hii kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne lakini sio wengi wanaoendelea na kidato cha tano na sita vlazima tuboreshe vyuo vyetu vya kati ili vijana ambao watashindwa kuendelea na masomo waende katika vyuo vya kati na ufundi,”alisema  

Waziri Jafo amesema serikali ya awamu ya sita imewekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo  itatanua wigo wa kuajiri vijana wenye umahili katika ufundi.

Alisema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na utahitaji vijana ambao wana ujuzi wa kutosha.

“Maeneo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa yanahitaji vijana ambao wamepata elimu ya ujuzi na sasa imeanza mchakato wa kufufua shirika la ndege ambapo hadi sasa kuna ndege 11 na itanunua nyingine hivyo wataitajika vijana wenye ujuzi wa katika  uendeshaji na ukarabati wa vifaa hivyo,”alieleza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda  amesema kuwa serikali ili kuendelea kukuza  bunifu za wanafunzi hawa kutoka vyuo vya ufundi serikali imepenga kuanza kuwapatia mikopo ya masomo ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi na hapo itapatikana idadi kubwa ya bunifu itakayoendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa katika sekta ya elimu.

Pia Prof.Mkenda amewataka NACTVET kufanya uchunguzi katika vyuo vyote vya ufundi ikiwa ni pamoja na VETA ili kuhakikisha vijana wanaoandaliwa wanakidhi katika soko la ajira ili kuhakikisha kuwa elimu wanayopewa inakwenda kuwasaidia.

"Niwatake mkafanye case study katika vyuo vyote vya ufundi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia katika soko la ajira narudia tena kuwa mkafanye hivyo maana wazazi wanalipa pesa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ili walete mafanikio katika nchi na familia kwa ujumla"Amesema Mkenda

Pia ameahidi kuwa serikali itafanya mpango wa maonyesho hayo kufanyika na upande wa Zanzibar ili kuendelea kudumisha Muungano. amewataka vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kujiunga na vyuo vya kati na ufundi.

WaziriJafo aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya Elimu ya Sayansi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET).

Waziri Jafo amesema takwimu za mwaka jana zinaeleza kuwa wanafunzi 173000 walimaliza kidato cha nne kati yao wanafunzi 90,000 waliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

“Leo hii kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne lakini sio wengi wanaoendelea na kidato cha tano na sita vlazima tuboreshe vyuo vyetu vya kati ili vijana ambao watashindwa kuendelea na masomo waende katika vyuo vya kati na ufundi,”alisema

Waziri Jafo amesema serikali ya awamu ya sita imewekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo itatanua wigo wa kuajiri vijana wenye umahili katika ufundi.

Alisema Tanzania inafanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere ambalo ujenzi wake unaendelea na utahitaji vijana ambao wana ujuzi wa kutosha.

“Maeneo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa yanahitaji vijana ambao wamepata elimu ya ujuzi na sasa imeanza mchakato wa kufufua shirika la ndege ambapo hadi sasa kuna ndege 11 na itanunua nyingine hivyo wataitajika vijana wenye ujuzi wa katika uendeshaji na ukarabati wa vifaa hivyo,”alieleza.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa serikali ili kuendelea kukuza bunifu za wanafunzi hawa kutoka vyuo vya ufundi serikali imepenga kuanza kuwapatia mikopo ya masomo ili kupata idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi na hapo itapatikana idadi kubwa ya bunifu itakayoendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa katika sekta ya elimu.

Pia Prof.Mkenda amewataka NACTVET kufanya uchunguzi katika vyuo vyote vya ufundi ikiwa ni pamoja na VETA ili kuhakikisha vijana wanaoandaliwa wanakidhi katika soko la ajira ili kuhakikisha kuwa elimu wanayopewa inakwenda kuwasaidia.

"Niwatake mkafanye case study katika vyuo vyote vya ufundi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa elimu ambayo itakwenda kuwasaidia katika soko la ajira narudia tena kuwa mkafanye hivyo maana wazazi wanalipa pesa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao ili walete mafanikio katika nchi na familia kwa ujumla"Amesema Mkenda

Pia ameahidi kuwa serikali itafanya mpango wa maonyesho hayo kufanyika na upande wa Zanzibar ili kuendelea kudumisha Muungano.

No comments:

Post a Comment