Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewahimiza madereva bodaboda na Bajaji wa mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kikao kitakachofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Mtaka ameyasema hayo hii leo July 23, 2022 Jijini Dodoma wakati akizungumza na madereva hao kuelekea katika kikao hicho kitakacho fanyika July 24 mwaka huu ambapo mgeni rasmi atakuwa Mh. Rais samia suluhu Hassan.
Amesema lengo la kuandaa kikao hicho ni kuonesha namna ambavyo kazi hiyo ni rasmi na inatambulika japo kumekuwa na watu wachache ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani na kujihusisha vitendo visivyo faa na kazi hiyo kuonekana ni ya kawaida.
“Lengo la kufanya hivi ni kuhitaji kuona ni kwa namna gani kazi hii mnayoifanya ni kazi rasmi na sio kazi ambayo mtu anaamka asubuhi kwa kuwa hana kazi ya kufanya, vilevile tuzungumze mambo yanayohusu usala wa kazi yenyewe,” alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodaboda na bajaji mkoa wa Dodoma, Keneth Chimoti amesema kuwa kila mmoja anatakiwa kuelewa kuwa ni wajibu wa
No comments:
Post a Comment