Watu saba wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha gari ndogo kugonga na mkokoteni uliokuwa unavutwa na ng’ombe katika Kijiji cha Lugala Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma leo Jumapili Julai 3, 2022.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Akizungumza kuhusu ajali hiyo Diwani wa kata ya Manzase mkoani Dodoma, John Mika amesema gari ndogo liligonga mkokoteni uliokuwa umebeba watu 12.
“Watu hao walikuwa wanakwenda kwenye mlima wa Lugala kwa ajili ya kuchimba udongo wanaotumia kufinyanga vyungu ndipo gari hilo likawagonga, ambapo watu sita walifariki hapohapo na ng’ombe wawili waliokuwa wakivuta mkokoteni walikufa,” amesema Mika.
Mika amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment