CHAMA CHA SKAUTI MNA KAZI KUBWA YA KUENDELEZA MALEZI MASHULENI-PROF.MKENDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 2, 2022

CHAMA CHA SKAUTI MNA KAZI KUBWA YA KUENDELEZA MALEZI MASHULENI-PROF.MKENDA

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Akizungumza wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ally Abdulgulam Hussein akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma
Skauti Mkuu wa Chama hicho ambaye amemaliza muda wake Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma
sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma
sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma

Na Okuly Julius Dodoma

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amewataka viongozi wapya wa Chama cha SKAUTI nchini kuhakikisha wanatumia nafasi walionayo kuimarisha Malezi mashuleni.

Tabia zingine mbovu zinazoibuka kwa sasa katika shule zetu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,utovu wa nidhamu na matukio mengine maovu ni kukosekana kwa michezo mashuleni ikiwemo mazoezi na mafunzo ya SKAUTI yenye lengo la kuimarisha maadili kwa wanafunzi.

Akizungumza wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI uliofanyika leo Julia 02,2022 jijini Dodoma Prof.Mkenda amesema kuwa kwa sasa matukio mengi ya utovu wa nidhamu na uvunjifu wa maadili mashuleni ni kutokana na kukosekana kwa michezo hivyo akawaagiza Uongozi wa Skuti nchini kuhakikisha wanashughulikia suala hilo.

"Niwatake kushughulikia tabia hizi mbovu ambazo chanzo chake kikubwa ni kukosekana kwa michezo mashuleni enezeni SAUTI mashuleni na kuhakikisha mnatoa malezi bora ili kuondoa haya matukio yanayosababishwa na malezi mabaya" Prof.Mkenda

Prof. Adolf Mkenda akizungumzia kuhusina na uchaguzi amesema kuwa leo anafungua ukurasa mpya kwa kuwataka viongozi wa bodi ya skauti waliochaguliwa kuhakikisha wanalinda jina hilo lisichafuliwe na kuyaenzi yale yote yaliyoanzishwa na watangulizi ili kuendelea kuimarisha Uadilifu na nidhamu katika chama hicho.

"Leo nafunga nz kufungua ukurasa mpya kabisa unaotafsiri nidhamu ,uadilifu katika chama hichi kwa kweli hatuwezi kuwa na skauti ambae kwa hiari yake na katiba yake imeamua kumweka Rais wetu kama mlezi, na kuweka viongozi wetu wastaafu Akiwemo Rais wetu Mstaafu wa awamu ya Pili mzee wetu Ali Hasan Mwinyi na viongozi wengine wa dini halafu tunafanya mambo ya mzaha mzaha nawaambia iwe Mwisho leo" amesema Prof.Mkenda

Mkenda amesema kuwa umefika wakati sasa kwa Uongozi wa Skauti kuonesha Uaminifu,uadilifu na nidhamu kwa kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizopo na kufungua ukurasa wenye kusadifu kilichopo ndani ya chama hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ally Abdulgulam Hussein amesema kuwa kuna kila sababu ya kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya Chama cha SKAUTI nchini ili kuonesha nafasi ya Zanzibar katika chama hicho huku akiomba mkutano mwingine utakaofuata kufanyika Visiwani Zanzibar.

Naye Skauti Mkuu wa Chama hicho ambaye amemaliza muda wake Mwantumu Mahiza amesema kuwa malengo makubwa ya chama hicho ni kujenga shule ya kimataifa ya mafunzo ya SKAUTI,kujenga vitega uchumi mbalimbali jijini Dodoma ambapo tayari wana hati ya kiwanja huku wakijivunia ahadi ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan aliyeahidi kutekeleza ahadi iliyokuwa imetolewa na Hayati Magufuli ya kuwapatia Bilioni 20 kwa ajili ya kufanya ujenzi huo.

"Viongozi mnaoingia madarakani niwaambie tu kuwa mna kazi ya kutekeleza malengo tuliyoyaanza ikiwemo kujenga shule ya kimataifa na kujaenga vitega uchumi hapa Dodoma kiwanya tayari tunayo na jambo la kushukuru ni kwamba Mhe.Rais amesema ataekeleza ahadi iliyokuwa imeyolewa na Mtangulizi wake Hayati Magufuli ya kutupatia Bilioni 20 kwa ajili ya kutekeleza huo mradi hivyo mfuatilie na kutekeleza,"Amesema Mwantumu

No comments:

Post a Comment