 |
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Akiongea na vyombo vya habari katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji akipitia baadhi ya machapisho yaliyopo kwenye banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji akieleza jambo kwa mmoja wataalamu waliopo kwenye banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
 |
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.) akizungumza jambo na mmoja wa wataalamu waliopo kwenye banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara akiambatana na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
 |
Mtafiti wa Shirika la Utafiti na Maendelea ya Viwanda (TIRDO) Bi.Jacqueline Mwandwa akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.) mara baada ya kutembelea banda la TIRDO akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara Prof. Godius Kahyarara katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (mwenye ushungi) akiuliza jambo kwa Mtafiti wa Shirika la Utafiti na Maendelea ya Viwanda (TIRDO) Bi.Jacqueline Mwandwa mara baada ya kutembelea banda la TIRDO katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sajini (Mb.) |
Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Katibu Mtendaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA), Mheshimiwa Wamkele Mene anatarajiwa kufungua Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) Julai 03,2022 katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri amebainisha hayo Julai 02, 2022 jijini Dar es Salaam alipotembelea katika viwanja vya maonesho hayo maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2022 na kutembelea majengo ya taasisi na kampuni mbalimbali zilizoshiriki maonyesho hayo.
Akiongea na vyombo vya habari, Waziri Kijaji amesema Septemba mwaka jana Bunge lilipitisha Mkataba wa Eneo Huru la Biashara, Afrika na Januari mwaka huu lilipelekewa taarifa ya kuonesha utayari wa Tanzania kuingia katika eneo hilo la biashara.
"Kawaida wananchi walizoea maonesho yanazinduliwa na kiongozi wa nchi lakini mwaka huu itakuwa ni tofauti, Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa fursa kwa sisi Watanzania kumkaribisha Katibu Mtendaji huyu na haya ni matokeo ya sisi kuingia huko katika ushirikiano," Amesema Dkt. Kijaji.
Aidha, Waziri Kijaji amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa maonesho hayo ambayo kwa kipindi hiki yameweza kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuweza kuvutia wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
"Tujitokeze kwa wingi kuja kumsikiliza mgeni wetu rasmi ambaye atatueleza fursa mbalimbali zilizopo katika soko hilo ili tuweze kuzitumia kikamilifu," aliongeza.
Hata hivyo Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara kuanza kuzalisha bidhaa zenye bora kwa ajili ya soko la Afrika na sio Tanzania pekee ili kuweza kujitangaza kwa nchi mbalimbali na duniani kote.
"Tunakoelekea ni kwamba Afrika inataka kuwa soko huru ambapo biashara zitatoka nchi moja kwenda nyingine bila vikwazo vyovyote. Tulichokubaliana katika Mkataba huo ni kwamba kila nchi iangalie sifa zipi za kipekee ambazo zikiweza kuchukuliwa na kutumiwa vizuri ndani ya Taifa hilo tunaweza kuzalisha kwa gharama nafuu na kuweza kuuza bidhaa zetu nje ya nchi. Aliieleza Dkt. Kijaji.
Aidha, Waziri Kijaji alifafanua kuwa wawekezaji wengi wanakuja nchini kwetu na hata Katibu Mtendaji huyu anakuja kuwaambia Watanzania Afrika tunakwenda kuwa soko moja, bidhaa zinazozalishwa Tanzania ziuzwe Afrika nzima.
No comments:
Post a Comment