NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI HAYA – MAJALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, July 23, 2022

NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI HAYA – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yatakayo fanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Julai 25, 2022, kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. Julai 23, 2022.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Askari Wastaafu waliopigana vita kuu ya Pili ya Dunia TLC, CHARLES LUBALA akizungumza na waandishi wa habari Julai 23,2022 kuelekea sherehe za siku ya mashujaa yatakayofanyika kitaifa Julai 25,2022 jijini Dodoma

Na Mwandishi wetu Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yatakayofanyika kitaifa Julai 25, 2022 Mkoani Dodoma

Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 23, 2022), baada ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo, katika viwanja vya Mashujaa Mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na maandilizi yaliyofanywa na kamati ya maadhimisho kitaifa kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

“Sherehe hii itafanyika kitaifa mkoani Dodoma na itaongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Viongozi wastaafu na viongozi wengine wa kitaifa.”

Waziri Mkuu amesema, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliridhia maadhimisho hayo yafanyike kitaifa mkoani Dodoma, lakini akaelekeza yafanyike nchi nzima kwa Wakuu wa Mikoa kuadhimisha siku hiyo kwa kwenda kwenye maeneo muhimu ya kumbukumbu kwenye mikoa yao.

“Kamati ya maadhimisho imefanya kazi yake vizuri sana kwa kushirikiana na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, eneo linafafana na tukio lenyewe, lakini maandalizi ya vikundi mbalimbali ikiwepo vyombo vya ulinzi na usalama vimeleta askari kwa ajili ya gwaride, na mwaka huu Jeshi la Uhamiaji limeanza kushiriki kikamilifu kwenye gwaride kuanzia kwenye tukio hili muhimu la mashujaa”

Aidha, Waziri Mkuu amevipongeza vyombo vya habari kwa namna ambavyo vimekuwa vikishiriki katika kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kitaifa na kwamba Serikali inathamini mchango huo.

“Serikali inawashukuru sana wananchi kwa namna ambavyo wanajitokeza katika matukio haya ya kitaifa na kujanza viwanja, tunaamini pia Julai 25 watajitokeza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Askari Wastaafu waliopigana vita kuu ya Pili ya Dunia TLC, CHARLES LUBALA amesema kuwa wamefurahishwa  na kurudishwa kwa maadhimisho ya siku hii ya sherehe ya mashujaa kwani imekaa zaidi ya miaka mitano bila kuadhimishwa.

LUBALA amemshukuru Mhe.Rais Samia kwa kurudisha maadhimisho hayo ikiwa ni fahari kubwa kwao kama mashujaa waliolipigania taifa tangu enzi za vita vya pili vya dunia huku akisema kuwa Mhe.Rais ameonesha kuwajali na kuthamini juhudi zao ndio maana akaamua kurudisha sherehe hizo.

"Kiukweli sisi kama chama cha maaskari wastaafu waliopigana vita kuu ya pili ya dunia ya mwaka 1949-1945 tumefarijika sana kuona Mhe.Rais Samia amerudisha tena hii siku ambayo itaadhimishwa kila mkoa ila kitaifa itafanyika hapa jijini Dodoma "amesema LUBALA 

KUTANA NA MZEE OMARY SHANGAZI MWENYE UMRI WA MIAKA 103 ALIYEPIGANA VITA KUU YA PILI YA DUNIA

Kutoka katika Uwanja wa Mashujaa Jamatini Jijini Dodoma Kwenye maandalizi ya Maadhimisho ya siku ya mashujaa OKULY BLOG pia Imefanya mazungumzo na Mzee Omary Shangazi mwenye umri wa miaka 103 ambaye ameshiriki vita kuu ya Pili ya Dunia vilivyopigwa kuanzia mwaka 1939 Hadi 1945 kati ya Ujerumani,Itali,Japani na Mataifa yaliyoshikamana nazo(Bulgaria na Hungari) dhidi ya Nchi nyingi za Dunia ziliitwa Mataifa ya ushirikiano ambazo ni Uingereza,Uchina,Urusi na Marekani

Mzee Omary ameeleza namna ambavyo alivyoshiriki vita hivyo mpaka kurudi nyumbani salama huku akiwa amewapoteza rafiki zake wengi ambao baadhi Yao waliuawa Kwa kulipuliwa na Bomu kwenye meli na Dikteta wa Kinazi Adolf Hitler wakati walipokuwa wanaelekea kwenye misheni za kivita.

"Nimewapoteza rafiki zangu wengi Sana wengine walitunguliwa ndani ya meli wakati wakienda Misiri kwenye Misheni umati wa watu wakazamishwa"amesema Mzee Omary Shangazi

Mzee Omary ambaye ni mkazi wa Arusha amesema kuelekea sherehe ya siku ya mashujaa anaiomba serikali iwaenzi na kuwapa heshima yao kwani ndio waliopigania taifa hili.

"Sisi kama Veterans tulisahaulika sana lakini namshukuru Mhe.Rais Samia kwa kutukumbuka tena na kuamua kurejesha maadhimisho haya na kwa hili nampongeza sana na niwaombe wanadodoma kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 25,2022 kushuhudia sherehe hizi"amesema mzee Omary


No comments:

Post a Comment