Na Okuly Julius-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii PINDI CHANA, amesema ili kukabiliana na migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu, serikali katika mwaka huu wa fedha wa 2022/23, itajenga vituo 19 kwenye maeneo yenye matukio mengi ili kuwadhibiti wanyama hao wakiwemo tembo.
Waziri CHANA, ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea vipaumbele vya mpango na bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2022/23 iliyoidhinishwa na bunge ya shilingi bilioni 670.85
Waziri huyo wa maliasili na utalii pia amegusia suala la ulinzi na usalama kwa wanyama hatarishi walio katika hatari ya kutoweka wakiwemo nyati weupe na faru katika hifadhi za taifa.
Kuhusu kampeni za kuhifadhi mazingira na upandaji miti katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo usimamizi wa misitu 57 yenye ukubwa wa hekta milioni 1.7 pamoja na mapitio ya mipango ya usimamizi wa misitu ya hifadhi 111
No comments:
Post a Comment