Na Okuly Julius-Dodoma
Uwepo wa Vifaa tiba vya kisasa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI vimesaidia kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa ya Mifupa, Ubongo, Uti wa mgongo na Mishipa ya Fahamu, na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya Awamu ya sita mbele ya waandishi wa habari Julai 28,2022 jijini Dodoma.
Dkt.Respicious amesema kuwa taasisi hiyo imenunua vifaa vya kisasa, zikiwemo; ICU Ventilators, Monitors, Vitanda na Ambulance ya kisasa (Vyenye thamani ya tsh billion 1.3 zilizotolewa na Serikali)
"Serikali imetoa Tsh Bilioni 4.4 kwajili ya ununuzi wa mashine mpya ya kisasa ya MRI na CT scan kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma hiyo kwa uhakika"Amesema Dkt.Respicious
Na kuongeza kuwa "Taasisi imenunua vifaaa vya chumba cha tiba Mtandao vya shilingi milioni 227 kwa ajili ya kuimarisha huduma hii nchini,Ununuzi wa Vipandikizi pia Serikali imetoa kiasi cha shilingi 4.2 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa Implants ili kukabiliana na changamoto la uhaba wa implants kwa wagonjwa" Dkt.Respicious
Aidha,Katika kipindi hiki cha mwaka mmmoja jumla ya wagonjwa 7,113 walifanyiwa upasuaji ikilinganishwa na wagonjwa 6,793 waliofanyiwa katika mwaka uliopita wa 2020/2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2%.
Upasuaji mbali mbali wa kibingwa uliofanyika ni pamoja na Kubadilisha nyonga 207,Kubadilisha magoti 182.Upasuaji wa mfupa wa kiuno 96
Pia Wagonjwa 200 wamefanyiwa upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu (Knee and Shoulder athroscopy) kati yao waliofaniwa mabega ni 32 na magoti ni 168,Wagonjwa 249 wamefanyiwa Upasuaji wa uti wa mgongo kwa kufungua eneo dogo (minimal invasive spine surgery), watoto 17 wamefanyiwa upasuaji wa kunyoosha vibiongo (scoliosis) na Wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (celebral aneurysm repair)
"Huduma za karakana ya viungo bandia, zimezidi kuimarika, katika kipindi hiki jumla ya viungo bandia 411 vimetengenezwa na kupitia kitengo hiki, Taasisi imeanzisha huduma mpya ya utengenezaji wa mkono wa umeme ambapo tayari wagonjwa watatu wameshahudumiwa, gharama zake ndani ya nchi ni Tsh milioni 15 na nje ya nchi ni milioni 30 mpaka 60" Amesema Dkt Respicious
Dkt.Respicious ameongeza kuwa taasisi hiyo inashiriki pia kwenye kuwajengea uwezo wataalamu wa hospitali kubwa hapa nchini ikiwemo Bugando, Mbeya, KCMC na hospitali ya kanda ya Benjamin Mkapa.
Amebainisha kuwa taasisi hiyo Kwa kushirikiana na chuo kikuu cha MUHAS imeendelea kufundisha wataalamu (mabingwa) wa mifupa, mishipa ya fahamu na upasuaji wa ubongo na imeendelea kua hospitali ya kufundishia ya College of Surgeons of East,Central and Southern Africa(COSECSA).
No comments:
Post a Comment