TUCTA YAWASILISHA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI JUU YA NYONGEZA YA MISHAHARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 27, 2022

TUCTA YAWASILISHA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI JUU YA NYONGEZA YA MISHAHARA

Rais wa shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya akizungumza na waandishi wa habari Julai 27,2022 Jijini Dodoma juu ya mapendekezo yao kwa serikali kuhusu nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limewasilisha mapendekezo yao kwa serikali kuhusu nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma huku wakidai kutorishwa na utaratibu uliotumika katika nyongeza hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 27,2022 Jijini Dodoma Rais wa shirikisho hilo Tumaini Nyamhokya amesema kuwa tayari wameshakabidhi mapendekezo yao kwa serikali kupitia kwa katibu mkuu wa Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora hivyo kwa sasa wanasubiri majibu ya serikali.

Amesema kuwa hakuna mtumishi yeyote wa umma aliyeridhishwa na nyongeza hiyo ya mshahara kwa sababu unakuta wale wenye kima cha juu cha mshahara wameongezwa asilimia sifuri nukta sita (0.6%) ukilinganisha na wale wa kima cha chini ambao wameongezwa Asilimia 23.3 jambo ambalo limeweka tofauti kubwa kati ya wale wenye kima cha juu na chini cha mishahara.

“Hakuna mtumishi yeyote aliyeridhishwa na huu utaratibu wa nyongeza ya mishahara huu utofauti kati ya kima cha chini na juu cha mishahara ni mkubwa mno haijawahi kutokea tofauti kubwa namna hii kutoka asilimia 23.3 hadi 0.6”Amesema Nyamhokya

Na kuongeza “Na tukumbuke mheshimiwa Rais alilenga kuongeza mishahara hakuwa amelenga kuwatoa watu kwenye daraja flani na kuwapeleka katika daraja lingine kwa hivyo kama ni nyongeza ya mshahara inatakiwa kugusa kila ngazi ya mshahara kwa mtumishi wa umma”Nyamhokya

Amezungumzia pia mbali tu na kutoridhishwa na nyongeza hiyo ya mishahara Nyamhokya amebainisha kuwa kuna baadhi ya kada za watumishi wa umma hazijaguswa kabisa na nyongeza hiyo kwa mfano watumishi wengi wenye mishahara binafsi,ATCL,TTCL na TRC hawajaguswa kabisa wakati na wenyewe ni sekta ya umma.

“Sio kama tumeridhishwa na hizi elfu sabini za kima cha chini hapana tunaweza tukawashukuru ila sio kiwango ambacho kinachoweza kumtoa mtumishi katika hali ngumu iliyopo kwa sasa kwa hivyo tunachotaka ni kuongezewa mishahara kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma iilivyokuwa inaongezwa”Amesisitiza Nyamhokya

Nyamhokya amesema kuwa katika mapendekezo waliyoyapeleka wamependekeza kuwa mshahara uongezwe kwa asilimia bila kuangalia kiwango cha fedha na kusema pia wamependekeza kuwa kima cha juu cha nyongeza ya mishahara kisipungue asilimia 15 wakati huyo wa kima cha chini akiwa na asilimia 23.3.

No comments:

Post a Comment