TUTAENDELEA KUONGEZA TIJA KATIKA SHULE ZINAZOMILIKIWA NA CCM- CHONGOLO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 15, 2022

TUTAENDELEA KUONGEZA TIJA KATIKA SHULE ZINAZOMILIKIWA NA CCM- CHONGOLO

Katibu Mkuu chama cha Mapinduzi[CCM] Daniel Chongolo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya watumishi wa taasisi za elimu zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi ya chama hicho julai 15,2022 jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ivumwe Sekondari Mwalimu Joseph K. Labre ambaye shule anayoiongoza imefanya vizuri katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dk. Edmund Mndolwa.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwanafunzi Philip Antipas Ng’eleshi kwa kushika nafasi ya 9 Kitaifa katika mtihani wa kidato cha sita  katika mchepuo wa PCB,katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dk. Edmund Mndolwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Wari Mwalimu Naomi Kikoti  wakati wa kikao cha tathmini na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi kilichofanyika leo Julai 15, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Dkt. Edimund Mndolwa,akizungumza  wakati wa kikao cha tathmini na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi kilichofanyika leo Julai 15, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani Shule za Jumuiya ya Wazazi Mwalimu Jacob Msigwa ,akizungumza  wakati wa kikao cha tathmini na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi kilichofanyika leo Julai 15, 2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Jumuiya Ya Wazazi Bw.Gilbert Kalima ,akizungumza  wakati wa kikao cha tathmini na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi kilichofanyika leo Julai 15, 2022 jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma 

Katibu Mkuu chama cha Mapinduzi[CCM] Daniel Chongolo amesema mpango wa chama hicho ni kuongeza tija katika kujenga mafanikio kwenye shule zinazomilikiwa na chama hicho.

Chongolo amebainisha hayo leo Juni 15,2022 jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa semina ya watumishi wa taasisi za elimu zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi ya chama hicho.

Chongolo amesema lengo la chama kuanzisha shule ni kuwezesha vijana wote kupata elimu iliyobora ambapo katika matokeo ya mtihani mwaka huu karibu asilimia 80 hadi 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na chama wamepata ufaulu wa daraja la kwanza na la pili huku mwanafunzi mmoja tu akipata ufaulu wa daraja la nne.

Aidha,ametoa wito kwa jumuiya kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wa shule ili heshima ya wakuu wa shule iendane na muda aliokaa katika shule.

Hata hivyo,amesisitiza kwa wakuu wa shule kuendelea kujenga nidhamu katika shule wanazoziongoza katika kuendelea kujenga heshima ya chama.

Katika hatua nyingine amebainisha kuwa heshima ya mwalimu ni matokeo bora hivyo amesisitiza kuwa awamu ijayo watatoa zawadi kulingana na kiwango cha ufaulu katika shule husika na kuwataka walimu kukaza buti katika ufundishaji.

Mwenyekiti jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi [CCM] Dkt.Edmundi Mndolwa amewataka watumishi katika taasisi za elimu zinazomilikiwa na chama kuacha kujihusisha na masuala ya siasa bali kujikita zaidi katika ufanikishaji wa utoaji wa elimu Bora.

Aidha,amesema kiwango cha ufaulu katika shule zinazomilikiwa na Chama zimeendelea kuimarika siku hadi siku kwani hakuna shule yoyote iliyopata daraja sifuri.

No comments:

Post a Comment