Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wajumbe wa Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi mkoa wa Dodoma kuwa wabunifu ikiwemo kutengeneza kitu kikubwa kitakochomfanya Mhe.Rais Samia kuendelea kujivuania dhamira yake ya kuanzisha majukwaa ya wanawake hapa nchini wakati akiwa makamu wa Rais.
Mtaka ameyasema hayo Julai 12,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya uongozi kwa wajumbe wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa wa Dodoma ambapo amewataka kuhakikisha wanajipanga kuandaa tukio kubwa kwa kuwaalika majukwaa toka mikoa yote ya uwezeshaji wa Kiuchumi kwa wanawake jambo ambalo litamfanya Rais kujivunia kazi kubwa aliyoifanya wakati akiwa makamu wa Rais.
"Nategemea mwaka huu mtandaa tukio kubwa ikiwezekana hata kama mtaomba tuwasaidie sawa tu ila liwe tukio kubwa ambalo litawakutanisha majukwaa kutoka mikoa yote na mumualike Mhe.Rais awe mgeni rasmi kuliko kukaa kimya mpaka mikoa mingine iwaalike nyinyi ni aibu kubwa"Amesema Mtaka
Na kuongeza "tumieni vizuri fursa hii ya kuwa makao makuu kwa sababu hapa kwa sasa kuna mambo mengi ya kufanya kama jukwaa na muhakikishie kila tukio litakalofanyika mkoani Dodoma nyinyi kama jukwaa muwe na Banda kuonesha bidhaa zenu na kufanya watu watambue kuwa Dodoma kuna nini"

No comments:
Post a Comment