![]() |
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Akizungumza leo Julai 04,2022 Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa usajili wa wakulima na mwongozo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea msimu wa 2022/2023 |
![]() |
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi wa usajili wa wakulima na mwongozo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea msimu wa 2022/2023 leo Julai 7,2022 Wilayani Chamwino mkoani Dodoma |

*******************
Na Okuly Julius Chamwino-Dodoma
Akizungumza leo Julai 04,2022 Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa usajili wa wakulima na mwongozo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea msimu wa 2022/2023 Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa sasa wakulima watajua ni aina gani ya Mazao,mbolea itakayotumika kutokana na majibu ya vipimo maalumu kupitia vifaa vya kupimia afya ya udogo hivyo kuwaondolea hasara wanayoipata kwa sasa ya kukosa mazao mengi kutokana na kutofahamu ni zao gani sahihi la kupanda katika udongo husika.
Aidha Bashe amewataka maafisa ugani kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa kufika kwa wakulima kwa sababu mpaka sasa hakuna kisingizio chochote cha kuwakwamisha kufanya hivyo kwani kila mmoja ameshapatiwa chombo cha usafiri (pikipiki) itakayoweza kumrahisishia kutekeleza majukumu yao.
"Niwatake maafisa ugani wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufika kwa wakulima mmekuwa mkifanya kazi kwa maneno naomba sasa twende kwa vitendo serikali imewekeza katika sekta ya kilimo na nia ya Mhe.Raisi ni kuona kilimo inakuwa kimbilio la kila kijana wa kitanzania na sio adhabu ndio maana serikali imetoa pikipiki elfu saba (7000) kwa ajili ya maafisa ugani nchi nzima"Amesema Bashe
Bashe amesema kuwa kupitia mfumo huo itasaidia kuwatambua wakulima wote nchini na namna ya kuwahudumia pia itakuwa ni rahisi kwani watafahamika kwa namba sio kwa makisio akiamini kwamba usajili huo ukikamilika basi hata ruzuku zinazotolewa na Serikali itatumika kwa usahihi.
"Wakulima wa nchi hii kwa miaka mingi hawajapata haki zao kwa mfano kwenye keki ya taifa mkulima hajajumuishwa kabisa wakati nae ni muwekezaji katika nchi hii na nia ya Rais wetu ni kuona kilimo kinapiga hatua kutoka hapa tulipo twende mbele"Amesisitiza Bashe
Na kuongeza "Usalama wa kwanza wa nchi hii anayehakikisha ni mkulima ambaye anahakikisha shibe na kutokomeza njaa hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama haviwezi kupambana na njaa ndio maana narudia tena mkulima ndio mtu anayetuhakikishia usalama wa nchi"
Mhe.Bashe ameongeza kuwa bila kupeleka fedha kwa wakulima hakuna kitu kitakachowezekana na ndio maana Mhe.Rais Samia ameamua kuelekeza Bilioni 150 katika sekta ya kilimo huku kukitarajiwa kuleta mapinduzi na kuondokana na kilimo cha mazoea
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.David Silinde amesema mfumo huu wa kusajili wakulima kidigitali utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa migogoro inayojitokeza wakati wa utoaji wa ruzuku ya mbolea .
Pia amongeza kuwa ajenda kuu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ni kuongeza mapato katika halmashauri na kupitia kilimo hilo linawezekana kama kutakuwepo na utekelezaji na ufuatiliaji mzuri katika sekta hii ya kilimo.
Amewataka Maafisa kilimo wote katika ngazi zote nchini warudi rasmi kufanya kazi zao za kitaalamu na kuacha kufanya kazi ambazo haziwahusu na kuwataka wakuu wote wa wilaya kuwafuatilia kwa ukaribu maafisa kilimo ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa wakulima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dr.Stephan Ngailo amesema kuwa ili kuweza kudhibiti bei za mbolea wameanza utaratibu wa kukusanya mahitaji ya mbolea ili kuweza kutangaza zabuni za BPS ambapo zoezi hilo mwisho wake ni Julai 7,2022 na baada ya hapo wataanza mchakato wa kupokea zabuni za BPS jambo ambalo litasaidia kudhibiti bei ya mbolea hapa nchini na agizo la serikali la kuwapunguzia makali wakulima katika manunuzi ya mbolea litakuwa limetekelezeka.
No comments:
Post a Comment