Na Mwandishi wetu Singida
Daraja hilo limejengwa kwa kutumia teknolojia rahisi ya mawe kwa gharama ya shilingi milioni 102. Ujenzi wa daraja hili ni sehemu ya kazi zilizofanyika katika Mkataba wa Matengenezo ya muda maalumu ya barabara ya Mwando - Miganga - Kinandili yenye urefu wa kilomita 12.39, kazi zote zimegharimu kiasi cha fedha milioni 444.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amewapongeza wakandarasi kwa ubunifu wa daraja hilo na kuagiza wapewe kazi ya ujenzi wa madaraja mengine.
Meneja wa TARURA mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia kuondoa changamoto ya mawasiliano iliyokuwepo kwa wananchi hasa kipindi cha masika.



No comments:
Post a Comment