Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewaagiza wakufunzi wote waliochaguliwa katika kutoa mafunzo kwa makarani wa sensa kuhakikisha wanazingatia uwadilifu wa taifa ili kuweza kumsaidia mh . Rais Samia katika kuyafikia yale ambayo yanakusudiwa kupatikana katika zoezi la sensa.
Agizo hilo amelitoa hii leo July 22,2022 Jijini Dodoma wakati alipoudhuria kikao Cha wakufunzi wa Sensa kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma, ambapo amesema kuwa ni vizuri kujuwa kwamba wamebeba dhamana kubwa na majukumu ya serikali ili kuhakikisha zoezi hilo la sensa linakwenda salama.
“Suala la sensa linalindwa na Sheria ili ikitokea karani akaharibu zoezi hili atahukumiwa adhabu ya kifungo Cha miezi sita na kuendelea, kwakuwa sensa ni jukumu ambalo linalindwa na sheria za nchi,”amesema Mtaka
Naye, Dk. Fatma Mganga katibu tawala mkoa wa Dodoma, amesema kuwa watakao sababisaha mkoa wa Dodoma kufanya vizuri katika Sensa ni wakufunzi ambao wataenda kuwafundisha makarani, ambao kila mkufunzi atakuwa anafundisha makarani 70.
Vilevile ameongeza kuwa zoezi la sensa ni nyeti katika ustawi wa taifa la Tanzania na kuwahasa kuwa waadilifu na kuzingatia maadili pamoja na kusimamia vizuri zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkufunzi mkuu wa sensa, Phausta Ntigiti amesema kuwa mafunzo hayo yalianza tangu tarehe 6 mwezi huu ambapo ni takribani siku ya 17 ambazo zimewahusisha washiriki 415 kutoka katika halshauri zaote za Jiji la Dodoma.
“Tulianza mafunza haya kwa kuwaelekeza wakufunzi hawa kuhusu Mambo muhimu ya kuzingatia kipindi cha sensa, ambapo walishiriki mafunzo haya wamekuwa wakiingia madarasani.
“Pia nitoe wito kwa wakufunzi wote kuhakikisha wanazingatia uwadilifu wa taifa na kuweza kumsaidia mh . Rais Samia katika kuyafikia yale ambayo yamekusudiwa kupatikana katika zoezi la hili lijalo la sensa,”amesema Ntigiti
Mafunzo hayo ambayo yameanza tangu tarehe 6 mwezi huu ambapo ni takribani siku 17, ambayo yanawahususha washiriki 415 kutoka katika halshauri zaote za Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment