CHIBEHE AIBUKA MWENYEKITI WA CCM KATA YA KILIMANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 19, 2022

CHIBEHE AIBUKA MWENYEKITI WA CCM KATA YA KILIMANI


Na Barnabas Kisengi Dodoma

Nathan Chibehe ameibuka kuwa mshindi nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma baada ya kumshinda aliyekuwa akitetea nafasi hiyo,Herry Kiwaya kufuatia chaguzi zinazoendelea kufanyika ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Jijini Dodoma uliofanyika katika Jengo la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Kata kilimani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini Said Kasote Amesema kuwa kura zilizopigwa ni kura 64 kura zilizoharibika ni kura 2 na kura halali ni kura 62.

Kasote amesema kuwa wagombea nafasi ya Mwenyekiti walikuwa ni Haruna Kifimbo alipata kura 1, Herry kiwaya alipata kura 27 na Nathan Chibehe ameibuka kuwa mshindi kwa kura 34 hivyo alimtangaza Nathan Chibehe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini JABIR SHEKIMWERI amewapongeza viongozi wote walio chaguliwa katika nafasi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment