FCS YATOA RUZUKU YA SHILINGI BILIONI NNE KWA AZAKI 89. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 15, 2022

FCS YATOA RUZUKU YA SHILINGI BILIONI NNE KWA AZAKI 89.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga akizungumza katika warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga (wa kwanza kushoto)katika picha ya pamoja wakiwa wameshikilia hundi katika warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma

NA WINNER MARAWITI -DODOMA

Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) limetoa ruzuku ya Shilingi Bilioni nne (4) kwa asasi za Kiraia (AZAKI) 89 Tanzania bara na Visiwani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji, elimu, afya na kilimo,usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, pamoja na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga wakati akizungumza katika warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata ruzuku jijini Dodoma.

Kiwanga amesema kuwa FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.

''FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao,"Amesema Kiwanga


Na kuongeza kuwa " Tutaweza kufanikisha malengo yetu kwa kuchangia maendeleo endelevu na shirikishi nchini Tanzania kwa kuimarisha uwezo, kugawana rasilimali, na ushirikiano wa kimkakati na AZAKIi, vikundi vya jamii pamoja na watendaji wengine wa maendeleo.''Kiwanga.

Nae ,Edna Chilimo Meneja Programu Utawala Bora FCS amezugumzia ruzuku mbalimbali ambazo FCS imetoa kwa AZAKI ikiwemo ruzuku ndogo, za kati na ruzuku za kimkakati.

''Tunafanya kazi na mashirikia madogo sana ambao wabia wanafika na pia tunafanya kazi na viongozi wa klasta za programu ambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa, tunafanya kazi na asasi za Kijiji, kata na wilayani, Wabia na mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu ili wawafikie wananchi waweza kuleta mabadiliko na maendeleo '' .Amesema Chilimo

Hata hivyo ikumbukwe kuwa FCS ni shirika huru la maendeleo, la Kitanzania lisilolenga kupata faida, ambalo hutoa ruzuku na huduma za kuzijengea uwezo asasi za kiraia nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment