JESHI LA ZIMAMOTO LATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA WA KAHAWA,CHAI NA MKONGE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 11, 2022

JESHI LA ZIMAMOTO LATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA WA KAHAWA,CHAI NA MKONGE.

Msemaji wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji SACF .Puyo Nzalayamaisi akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 11,2022 jijini Dodoma

Na Okuly Julius-Dodoma

Jeshi la zimamoto na Uokoaji limefuta tozo za ukaguzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mashamba ya Kahawa, mashamba ya chai na mkonge ambapo kabla ya kufutwa kwa tozo hizo gharama za ukaguzi zilikuwa zinaanzia laki tano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 11,2022 jijini Dodoma Msemaji wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji SACF .Puyo Nzalayamaisi amesema kuwa mabadiliko ya tozo za ukaguzi wa usalama dhidi ya majanga ya moto katika majengo na maeneo mbalimbali pamoja na utaratibu wa ukusanyaji wa tozo hizo zimeanza mwezi Julai,2022.

Ameongeza kuwa pamoja na mabadiliko ya utaratibu wa ukaguzi,jeshi hilo limefanya pia mabadiliko ya gharama za tozo katika maeneo mengi mfano maduka, viwanda, makazi, ofisi, shule, nyumba za kuishi, usomaji wa ramani pamoja na gharama za usajili wa makampuni yanayojishughulisha na utoaji huduma za kuuza vifaa, uwekaji wa vifaa vya kuzima moto pamoja na mifumo ya uzimaji moto.

"Pamoja na kushuka kwa gharama za tozo kuna maingizo mapya ya tozo ikiwa ni sehemu za karakana, vituo vya usafirishaji na wanaofanya biashara ya kufua nguo 'dry cleaner'"Amesema SACF .Puyo Nzalayamaisi

No comments:

Post a Comment