Katibu tawala ataka matokeo chanya ruzuku za mbolea - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 24, 2022

Katibu tawala ataka matokeo chanya ruzuku za mbolea


Na Mwandishi wetu-Kilimanjaro 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Willy L. Machumu ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha ruzuku za mbolea zinazotolewa nchini ziwe na matokeo chanya.

"Tuyapime na yaonekane tusitoe ruzuku ili mradi tumetoa" Machumu alikazia.

Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na timu ya wataalamu kutoka TFRA waliofika ofisini kwake kwa lengo la kueleza uwepo wao wa kutoa elimu juu ya mpango wa ruzuku kwa watendaji, waingizaji na mawakala wa mbolea wa mkoa huo.

Pamoja na kauli hiyo, Machumu aliwataka wataalamu hao kutekeleza majukumu yao kwa utulivu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Pia alishauri wakati wowote wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa majukumu washauriane na viongozi ili kuwa na muda mzuri wa kuweka taratibu sawa na baadaye kuendelea na zoezi kwa uhakika zaidi. "Viongozi wanashaurika hivyo tuwashauri pale inapobidi tusikurupuke" Machumu aliongeza.

Aidha, Katibu Tawala Machumu alimtaka Katibu Tawala Msaidizi Masuala ya Uchumi Mkoani hapo, Dkt. Vedast Makota kuuelewa vyema mfumo huo wa utoaji wa mbolea za ruzuku ili awe mwalimu wa wengine wakati wa usimamizi na utekelezaji wa mpango huo.

Akielezea nia ya kufika mkoani hapo, Kaimu Meneja wa TFRA kanda ya Kaskazini Gothard Liampawe amesema ni kutoa elimu ya mfumo wa kidigitali wa utoaji wa mbolea za ruzuku kwa watendaji wa serikali, waingizaji na mawakala wa mbolea wa mkoa huo ili wakulima waendelee kununua mbolea kupitia mfumo huo.

No comments:

Post a Comment