"PESA ZA MFUKO WA VIJANA ZAKOMBOLEWA NA MWENGE WA UHURU, ZITANUFAISHA VIJANA WOTE TENA" KATAMBI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 16, 2022

"PESA ZA MFUKO WA VIJANA ZAKOMBOLEWA NA MWENGE WA UHURU, ZITANUFAISHA VIJANA WOTE TENA" KATAMBI



Na Bilson Vedastus Dodoma

WIZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana kazi na Ajira, Patrobas Katambi, amesema hadi kufikia Agost 14 mwaka huu Mwenge wa Uhuru tayari umeshatembelea jumla ya Halmashauri 135 kati ya 195 zilizopangwa kutembelewa.

Pia amesema umekagua, kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali 941 yenye thamani ya Sh bilioni 551.7 kati ya hiyo miradi 64 yenye thamani ya Sh. Milioni 847.6 ndiyo iliyobainika kuwa na dosari ikiwemo kukosa nyaraka na changamoto mbalimbali za kiufundi.

Katambi ametoa taarifa hiyo Wilayani Bahi eneo la Bahi Sokoni mkoani Dodoma wakati wa makabidjiano ya Mwenge Kati ya uongozi wa mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Singida.

Ameeleza miradi hiyo na Kwa Kasi na maelekezo ya wakimbiza Mwenge waendelee kuirekebisha ili kuwa Sawa Sawa, mwenge wanuhuru no jicho la Rais, Samia Suluhu Hassan hivyo miradi itakapokuwa na dosari hawatasita kufichua.

Naibu Waziri huyo amesema, wakimbiza Mwenge huo wameweza kuhamasisha suala la lishe na kutoa elimu ya hamasa kwa wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi ikiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kwani Sensa ni Afya, ni barabara, zahanati Sensa ni maendeleo ndio uchumi, Sensa ni elimu, Sensa ni kila kitu hivyo ni muhimu Sana mana haiacho chochote.

Akizungumzia fedha za mfuko wa maendeleo aliwapongeza wakimbiza Mwenge kwa kufanikiwa kukusanya fedha hizo zikizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa vijana zaidi bill 847.6 na kuzirejesha serikalini.

Katambi amesisitiza kuwa Anaimani mikoa yote ikiwemo Dodoma watawasilisha Fedha hizo na kuhakikisha Fedha hizo zikizotolewa na Serikali zinarejeshwa Serikali kuu.

"Wewe fanya mchezo utakwenda na mwenge, usipotekeleza majukumu yako na kupunguza uzembe ubadhilifu, utaufuata nya, "hivyo kila mmoja nasisitiza awe makini katika eneo lake,"alisema Katambi

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba wamekabidhiana hati ya makabidjiano ya mwenge wa Uhuru leo katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma baadabya kumaliza mbio zake mkoani Singida ambapo sasa itaanza kukimbizwa rasmi katika mkoa wa Dodoma ndani ya Wilaya zake Saba.

Akipokea mwenge huo Mkuu wa mkoa wa Dodoma alisema Mwenge huo ukiwa ndani ya mkoa wa Dodoma utakimbuzwa umbali km 1162 na kwamba jumla miradi 39 yenye thamani Sh.bilioni 14.1.56 itazinduliwa.

Pia alisema Mwenge utaeneza jumbe mbalimbali ikiwo ujumbe wa Sensa ya watu na makazi wilaya Saba na Halmashauri name za Dodoma Hadi Agost 24 mwaka huu, mpaka watakapo ukabidhi Morogoro.

Mkuu wa huyo wa mkoa alibainisha kuwa Mwenge huo utakimbuzwa kwa muda wa siku 8 katika mkoa wa Dodoma katika kwenye Halmashauri zote 7.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge huo kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa, Sahil Gelaruma aliutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha miradi yote itakayokaguliwa kuandaliwa vyema ikiwa na nyaraka zote muhimu na kwamba miradi ambayo haitakuwa na nyaraka hizo haitakaguliwa.

Alisema zipo fedha zikizotolewa na Serikali kuu na kupelekwa katika halmashauri zote nchini kwa ajilinya Mfuko wa vijana na Kwa mkoa wa Dodoma jumla ya Sh. Milioni 150 hazijarejeshwa Serikali kuu.

"Mwenge wa Uhuru unaagiza halmashauri hizo kurejesha Fedha hizo haraka kabla mwenge wa uhuru haujapita katika halmashauri zao, mwenge wa Uhuru hautaondoka Dodoma mpaka fedha hizo zitakaporejeshwa,"alisisitiza kiongozi huyo.

Kiongozi huyo alisema mikoa yote waliyopita wamehakikisha fedha hizo za mfuko wa vijana zikizotolewa na halmanshuri kuu zimerejeshwa Serikali kuu hivyo Itakuwa ni Jambo la ajabu kama Dodoma hawatafanikisha hilo.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Ashanti Kijaji, akizungumza Sensa ya watu na makazi alisema, ni Sensa ya aina Yale no Sensa ya kidigital kwa maendeleo ya watu wote wajitokeze Kwa wingi ili kupata takwimu sahihi za uwekezaji katika suala zima la viwanda na biashara.

Agosti 17 mwaka huu Mwenge utakimbuzwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma baada kukamilisha mbio zake katika wilaya ya Bahi.

No comments:

Post a Comment