![]() |
| Muonekano wa Soko jipya la Machinga Complex lilijengwa katika eneo la Bahi Road jijini Dodoma ambalo ifikapo tarehe 23,Septemba 2023 litaanza kutumika na wafanyabiashara wadogo wadogo. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Agizo hilo limetolewa Leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukamilika kwa soko Hilo ambalo Lina uwezo wakuchukua wafanyabiashara 5000.
Ambapo amesema lengo la Jiji la Dodoma ni kuhakikisha Mji huo unakuwa katika Mpangilio maalum huku akitangaza siku maalum ya usafi baada ya wamachinga kuhama kuwa ni Septemba 24,2022.
"Tunaposema usafi tuna maanisha kuondoa kila kitu ambacho hakipo kwenye mpangilio mzuri hivyo niwaombe muwatangazie vizuri kabisa tutakuwa na usafi mkubwa wenye hadhi ya jiji letu,"Amesema Mafuru
Mafuru ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha machinga wote wa Jiji la Dodoma wanapata nafasi ya kufanya Biashara katika Soko hilo huku akibainisha kuwa litakuwa eneo salama sana kwa wamachinga pamoja na bidhaa zao.
Aidha amebainisha kuwa Jiji limekuwa likitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo Kila Mwaka huwakopesha kiasi Cha Shilingi Bilioni 1 na tayari wametenga bilioni 5 kwaajili yakuwakopesha wafanyabiashara hao.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema kuwa hawajafunga milango ya uhakiki kwa wamachinga hivyo kama kuna ambaye hajasajiliwa mpaka sasa ofisi ipo wazi kwa ajili yao.
"Mpaka tunapozungumza hapa sijapokea malalamiko yeyote kama kuna mfanyabishara mdogo mdogo ambae hajasajiliwa au kuhakikiwa na kama yupo ofisi zipo wazi na kwa uzuri zaidi tumefungua ofisi pia pale Machinga complex hivyo huduma zote mtazipata palepale,"Amesisitiza Mafuru



No comments:
Post a Comment