KAMATI YA BUNGE YAPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 5, 2022

KAMATI YA BUNGE YAPAZA SAUTI VITENDO VYA UKATILI

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akitoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha robo mwaka, Julai hadi Septemba mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju, akifafanua jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha robo mwaka Julai hadi Septemba mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kipindi cha robo mwaka Julai hadi Septemba mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Taufiq akichangia katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kipindi cha robo mwaka Julai hadi Septemba mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati wa kikao cha kuwasilisha wa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kipindi cha robo mwaka Julai hadi Septemba mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.

             (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM)

Na WMJJWM Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kulivalia njuga suala la vitendo vya ukatili vinavyoshamiri ndani ya jamii kwa kuja na mipango na mikakati thabiti ya kupambana na janga hilo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wakati wa kikao cha Kamati hiyo kujadili utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kilichofanyika Septemba 05, 2022 jijini Dodoma.

Mhe. Nyongo amesema kuwa Serikali iweke mipango na mikakati ya kuweza kulifanya suala la ukatili wa kijinsia linakuwa agenda ya Kitaifa ili kila mtu zikiwemo Taasisi za Kiserikali, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi zikishirikiana kwa pamoja zitaweza kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

"Suala hili Serikali iseme ni janga la Taifa ili twende pamoja kuhakikisha tunapambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa dhidi ya Wanawake na Watoto ndani ya jamii zetu" alisema Mhe. Nyongo

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Wizara, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema katika kukabiliana na changamoto ya vitendo vya ukatili katika jamii Wizara imeendelea kuelimisha jamii ambapo, baadhi ya wananchi wameelewa na kuhamasika kuhusu ukatili wa kijinsia na watoto na Wizara imeunga mkono Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) kwenye Mikoa yote 26 ya Tanzania. 

Mhe. Gwajima amesema, Kampeni hiyo inaratibiwa na kusimamiwa na Wizara ikishirikiana na wadau mbalimbali na mpaka sasa wananchi 8,319 wamejiunga na kampeni hii.

Ameongeza kuwa Wizara inaendelea kujenga uelewa wa jamii kuhusu haki, ulinzi na malezi ya watoto, madhara ya ukatili wa kijinsia, kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa jamii na mchango wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya Taifa kupitia vyombo vya habari, mikutano na makongamano.

 “Wizara imeendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi wa wanawake na watoto kwa ajili ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika Vyuo vya Elimu ya Juu, vya Kati, Shule za sekondari na Shule za Msingi ambapo madawati 43 yameanzishwa “alisema Dkt Gwajima

Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amefafanua kuwa, Wizara itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo Mashirka Yasiyo ya Kiserikali, Taasisi za Dini na sekta binafsi ili kuhakikisha jamii inapata uelewa juu ya madhara na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto.

Akichangia wakati wa wasilisho hilo Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Taufiq ameiomba Wizara kuweka nguvu na mkazo kwenye kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili wa kijnsia kwani vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu ikiwemo ndugu baba, mama, mke au mume hivyo jamii ikihusishwa kwa karibu ndio yenye kutoa ufumbuzi wa kukabiliana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment