KUELEKEA SIKU YA WAZEE DUNIANI TUWATHAMINI,TUWAHESHIMU,TUWATUNZE,TUWAJALI,LAKINI PIA TUYAENZI MEMA YAO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 29, 2022

KUELEKEA SIKU YA WAZEE DUNIANI TUWATHAMINI,TUWAHESHIMU,TUWATUNZE,TUWAJALI,LAKINI PIA TUYAENZI MEMA YAO.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akizungumza leo Septemba 29,2022 Jijini Dodoma kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wazee yatakayofanyika kitaifa Oktoba 3,2022 katika uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

"Ustahimilivu na mchango wa Wazee ni muhimu kwa Maendeleo ya Taifa" hii ni kauli mbiu itayoibeba maadhimisho ya siku ya Wazee ambapo kwa mwaka huu kitaifa itafanyika septemba 3,2022 katika viwanja vya mashujaa jijini Dodoma.

Kwa mara ya mwisho maadhimisho haya yalifanyika kitaifa mkoani Mtwara mnamo Mwaka 2019 ambapo mwaka 2020 na 2021 maadhimisho hayo yalifanyika katika ngazi za Mikoa huku Wizara ikishiriki Mkoani Dodoma katika Halmashauri za Kondoa na Mpwapwa, sababu kubwa ni kutokana na changamoto ya UVIKO 19.

Ikumbukwe kuwa mnamo December 14,1990, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Azimio Namba 45/106 ulitenga siku ya Oktoba Mosi (1) kuwa siku ya Wazee.

Hivyo Tanzania nayo ikaungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa wazee na tangu kuanza kwa maadhimisho hayo mnamo mwaka 1991,Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuadhimisha siku hiyo.

Lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha jamii inajengewa uelewa na kutiwa hamasa kuhusu kulinda haki,ustawi na maslahi ya wazee hapa nchini.

Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa siku hiyo itakwenda sambamba na utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo kupima afya, elimu kuhusu chanjo ya uviko, pamoja na msaada wa kisaikolojia na ushauri nasaha kwa wazee na wananchi wote.

Dkt.Gwajima amesema kuwa kilele cha Maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Pia Dkt.Gwajima amesema kuwa siku moja kabla ya kilele cha siku ya wazee kutakuwa na Kongamano ambalo madambalimbali zitajadiliwa zinazolenga afua kwa wazee ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya za wazee pia ,elimu ya ujasiriamali ili wazee waweze kupata ujuzi utakao wawezesha kufanya shughuli ndogondogo za uzalishaji zitakazo wasaidia kuchangamsha miili yao pamoja na kujiongezea kipato ili kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Pamoja na hayo Dkt.Gwajima ametoa rai kwa Mikoa yote hapa nchini kuhakikisha wanaadhimisha siku hii na kutoa huduma mbalimbali kwa wazee pamoja na elimu kuhusu haki,matunzo na ulinzi kwa wazee.

"Ni imani yangu kwamba huduma na elimu itakayotolewa katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho na siku ya Maadhimisho zitasaidia kujenga uelewa mpana kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwaenzi wazee wetu kwani WAZEE NI TUNU YA TAIFA TUNATAKIWA KUWAENZI NA KUWATUNZA," Amesema Dkt.Gwajima

Pia amewataka viongozi wote katika ngazi zote na wanajamii wote kwa ujumla kuwaunga mkono wazee wote kwa kushiriki katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment