LISHE BORA SHULENI INAWAJENGEA WANAFUNZI UTULIVU WA AKILI WAWAPO DARASANI-KIPANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 15, 2022

LISHE BORA SHULENI INAWAJENGEA WANAFUNZI UTULIVU WA AKILI WAWAPO DARASANI-KIPANGA

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga Akizungumza leo Septemba 15,2022 Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Utiaji Saini Fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga (kushoto) akisaini Fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni leo Septemba 15,2022 Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Utiaji Saini Fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni na (kulia) ni Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),Sarah Gordon-Gibson akishuhudia tukio hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga (kushoto) na Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),Sarah Gordon-Gibson (Kulia) wakikabidhiana fomu ya makubaliano ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni baada ya kutiwa saini katika hafla iliyofanyika leo Septemba 15,2022 Jijini Dodoma
Baadhi ya wa Shiriki waliohudhuria hafla fupi ya Utiaji Saini Fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni iliyofanyika leo Septemba 15,2022 Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema kuwa ili kupata matokeo mazuri ya elimu ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora shuleni ili kuwajengea wanafunzi afya bora na kupata utulivu wa akili wawapo madarasani.

Katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji, upatikanaji wa matokeo mazuri ya elimu hutegemea afya aliyonayo mwanafunzi huku Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ikifafanua upatikanaji wa huduma muhimu katika shule na vyuo ikiwemo huduma ya chakula bora, maji safi na salama na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanafunzi.

Akizungumza leo Septemba 15,2022 Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Utiaji Saini Fomu ya kujiunga na Muungano wa Chakula Shuleni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipanga amesema kuwa Pamoja na kuwepo kwa sera hiyo, utoaji wa huduma ya chakula shuleni umekuwa ukitekelezwa katika shule kwa namna na viwango tofauti.

" Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inafafanua kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu katika shule na vyuo ikiwemo huduma ya chakula bora, maji safi na salama na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanafunzi ndio maana leo kwa pamoja hapa tunatia saini fomu ya kujiunga na MuunganowaChakulaShuleni nia ni ile ile ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri na kupata matokeo mazuri . "Amesema Mh.Kipanga .

Mh.Kipanga amesema Mwezi Oktoba, 2021 Wizara ya Elimu ilizindua Mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa Wanafunzi wa Elimumsingi ili kuweka utaratibu wa kitaifa ambao utawezesha wanafunzi kupata huduma hiyo muhimu.

"Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakinufaika na wengine kukosa huduma hiyo muhimu sasa naamini kupitia Muungano huu utasaidia kuziba yale mapengo yaliyokuwepo na wanafunzi sasa hawatakuwa na sababu yeyote ya kutopata matokeo mazuri" Amesema Mh.Kipanga.

Katika hatua nyingine ,amesema kuwa utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni ni suala mtambuka linalohitaji ushiriki wa sekta na wadau mbalimbali na kwa upande wa Tanzania, Muungano huu, ni jukwaa muhimu la kupata uzoefu wa namna nzuri ya kutekeleza mpango wa
chakula shuleni kwa kushirikisha jamii na kufahamu wadau ambao tayari wapo kwenye muungano na wangependa kufadhili shughuli mbalimbali za kuwezesha upatikanaji wa
chakula shuleni.

"Kujiunga na muungano huu kutawezesha wadau wetu wa maendeleo,
mashirika yasiyo ya kiserikali, Makampuni binafsi pamoja na vyombo vya Habari, kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa chakula na lishe shuleni"Amesema Mh. Kipanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),Sarah Gordon-Gibson amesema kuwa moja ya njia ya kufikia malengo kwa taifa lolote Duniani ni lazima kuwekeza kwa watoto hivyo ili kufikia huko lishe ni eneo linalohitaji maboresho makubwa.

"Ukitaka kuwekeze kwa namna yeyote ile ni lazima uwekeze kwa watoto na hapo lishe bora haiepukiki mashuleni ndio maana sisi kama Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Ili kuhakikisha kwamba kila mtoto ana fursa ya kukua, kujifunza na kustawi, kundi la Nchi Wanachama na washirika waliunda Muungano wa Kimataifa wa chakula Shuleni,"Amesema Sarah

Na kuongeza kuwa Muungano wa kimataifa wa chakula shuleni Ilianzishwa wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mifumo ya Chakula ya 2021 na, hadi sasa, inaundwa na nchi 67 na washirika 68 na inaongozwa na Nchi Wanachama waanzilishi na kuungwa mkono na sekretarieti inayoendeshwa na WFP,"Ameongeza Sarah

Naye Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Mpango Chakula Duniani (WFP) Dodoma Mina Sitta amesema ni Muungano wa kimataifa wa chakula shuleni ni jukwaa la kuhakikisha nchi zote duniani ifikapo 2030 kila mtoto anapata angalau mlo mmoja shuleni.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Suzan Nusu amesema tukio la kutia saini kujiunga na muungano wa chakula Shuleni limeonesha dhamira ya dhati ya Serikali kuhakiksha watoto wote wanapata chakula shuleni na kwamba wanahidi kusimamia utekelezaji wake ili watoto wasome bila changamoto zozote.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi mbalimbali wa shule za Msingi na Sekondari za Mkoani Dodoma ambao wameshiriki katika hafla hiyo wameipongeza Serikali kwa kujiunga na muungano wa Chakula Shuleni  kwani utawawezesha kupata chakula shuleni na kuwaepusha na vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao za kupata elimu.

Muungano wa Kimataifa wa chakula Shuleni inalenga kusaidia serikali na washirika wao kuboresha ubora wa chakula cha shule na kuimarisha mifumo ya chakula shuleni, kwa njia ambayo inalingana na mazingira ya ndani, na ambayo inakuza ushiriki wa ujuzi na mbinu bora ambapo lengo kuu ni kutoa chakula chenye lishe kwa watoto wote kila mahali ifikapo mwaka wa 2030, na hivyo kuwa kichocheo kikuu cha kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu.


No comments:

Post a Comment