Na Mwandishi wetu - Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amezindua Mpango Mkakati wa Vijana wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Nchini.
Akizindua Mpango huo Jijini Dodoma Bwa.Mmuya amesema mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 7.0 kwa mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 4.7 kwa mwaka 2017.
Mmuya amesema Pamoja na mafanikio hayo ni vyema Kuongeza jitihada katika kuhamasisha upimaji wa VVU ili kufikia malengo ya Kitaifa ya 95 kwa mwaka 2025 na ifikapo mwaka 2030 iwe imefikia sifuri (0 ).
Nitoe wito kwa wadau wote wanaotekeleza afua za mwitikio wa UKIMWI kufanya tathimini ya mwelekeo wa utekelezaji katika kufikia malengo ili palipo na changamoto tuweze kurekebisha na kuimarisha na penye mafanikio tuongeze nguvu na Mipango yetu ya kimkakati ionyeshe wazi jinsi tutakavyofikia Tanzania isiyo na UKIMWI ifikapo mwaka 2030,alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Pia Naibu katibu Mkuu Mmuya amesisitiza kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambao ni waratibu wa shughuli za UKIMWI ndani ya mikoa wawe chachu ya utekelezaji wa maelekezo hayo ndani ya mikoa yao.
Niwasisitize watumishi wa Serikali kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkasimamie na kuratibu vyema Halmashauri zote kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) tuweze kutimiza vyema azma yetu,Alisisitiza
Aidha amesisitiza Uhamasishaji Kwa wanaume kuhakikisha wanatumia huduma za VVU na upimaji kwa ajili ya kufikia 95 ya kwanza pamoja na kufuatilia vijana wakike watumie huduma za VVU ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kutokomeza ukatili wa kijinsia.




No comments:
Post a Comment