WABUNGE WAUPA TANO MPANGO WA KUIJENGA UPYA MUHIMBILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 4, 2022

WABUNGE WAUPA TANO MPANGO WA KUIJENGA UPYA MUHIMBILI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Mbunge wa Maswa Mashariki Mh. Stanslaus Nyong’o, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa fedha za Uviko 19 yenye thamani ya TZS 11 Bil zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya, Mh. Dkt. Godwin Mollel (katikati), Mh. Stanslaus Nyong’o, Prof. Lawrence Museru na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, wakisikiliza maelezo kuhusu kitengo Huduma ya dharura kwa watoto kutoka kwa Dkt. Juma Mfinanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Muhimbili.
Mjumbe wa wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mh. Salma Kikwete akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa.

Na Mwandishi wetu-Dodoma 

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wameafikiana na mpango kabambe wa kuiendeleza na kuijenga upya Hospitali ya Taifa Muhimbili unategemea kugharimu zaidi ya TZS 600 Bil unaolenga kuboresha hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo ya taifa yenye hadhi ya ubingwa wa juu nchini.

Wakizungumza leo, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa ufadhili wa fedha za Uviko 19 yenye thamani ya TZS 11 Bil zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita katika hospitali hiyo, wabunge hao wamesema mpango huo utasaidia sana kuboresha hali ya utoaji huduma na kwamba utaipa hospitali hadhi yake kama hospitali ya taifa tofauti na sasa ambapo majengo mengi ni chakavu licha ya huduma bora na za kibingwa zinazotolewa na hospitali hiyo.

“Tumesikia mpango wa ujenzi wa Hospitali na sisi tupo pamoja na nyinyi na kama kamati tutaendelea kuisimamia serikali itenge pesa hizo na kuhakikisha tunajenga upya hospitali mpya ili wananchi wapate huduma, na kwa kweli katika maeneo ambayo tumetembelea tumeridhishwa na hali utoaji huduma na kwa hilo tunaipongeza sana wizara pamoja na uongozi wa Muhimbili” amesema Mh. Slanslaus Nyong’o ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Wawi Mh. Kassimu Khamis amesema kuwa kwa hadhi ya huduma za kibingwa zinazotolewa Muhimbili ni wakati sasa wa kuwa na majengo ya kisasa yanayoendana na hadhi ya hospitali ya taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mh. Salma Kikwete ameshauri kuwa utekelezaji wa ujenzi mpya wa hospitali uende sambamba na utunzaji wa historia ya hospitali ili iweze kunufaisha vizazi vijavyo.

Kuhusu hali ya utoaji huduma wabunge hao wamesema kuwa wameridhishwa sana na hasa uanzishwaji wa huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa hazipatikani nchini ikiwemo tiba radiolojia ambayo imesaidia serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

“Wataalamu wa Muhimbili wanajitoa sana katika kuwasaidia wananchi, mimi niliopigwa kweli kweli na Uviko 19, nilikuja kuponea hapa, nakiri nilipata huduma bora na ya kiwango cha juu sana, nawaomba watoa huduma wetu waendelee kuwa na moyo huo huo wa kuwasaidia wananchi” amesema Mh. Husna Sekiboko Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mh. Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa wizara imeshapokea mpango wa kuijenga upya Muhimbili na kwamba serikali ya awamu ya sita ipo tayari kuutekeleza. Kuhusu miradi ya fedha za UVIKO-19, amesema kuwa itaboresha sana hali ya utoaji huduma na kupunguza rufaa za wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.

"Nyie wenyewe mmeona uwekezaji ambao Mh. Rais Samia ameufanya kwa hospitali ya Muhimbili , amewekeza wa 11 Bil katika idara moja ya Radiolojia, ambao unakwenda kusaidia kuokoa zaidi ya TZS 100 Mil ambazo zingetumika kwa mtu mmoja kwenda kutibiwa nje ya nchi na haya ndio matunda ya kodi zetu", amesema Dkt. Mollel

Awali akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa chini ya miradi hiyo vyumba vya wagonjwa mahututi 4, vyumba vya wagonjwa uangalizi maalumu (HDU) 21, kitengo cha magonjwa ya dharura kwa watoto na kitengo cha wajawazito wanaohitaji uangalizi maalumu vilikarabatiwa.

“Pamoja na ukarabati lakini asilimia 70 ya fedha hizo zimetumika mkununulia vifaa vya radioloji ambavyo ni Mashine za CT Scan, MRI na Angio Suite” amesema Prof. Museru.

No comments:

Post a Comment