CPB KUANZA KUZALISHA MAFUTA YA KUPIKIA KWA KUTUMIA PUMBA ZA MPUNGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 24, 2022

CPB KUANZA KUZALISHA MAFUTA YA KUPIKIA KWA KUTUMIA PUMBA ZA MPUNGA

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB),Dkt. Anselm Moshi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Na Okuly Julius-Dodoma

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB),imesema ina mpango wa kuzalisha mafuta na kuni kupitia pumba za Mpunga ili kupunguza uharibifu wa mazingira na gharama za maisha kwa wananchi.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB),Dkt. Anselm Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Dkt. Moshi amesema kuwa kwasasa wapo katika upembuzi yakinifu katika kuongeza thamani ya zao la mpunga ili kuweza kuzalisha mafuta yatokanayo na pumba za mpunga.

Hata hivyo Dkt.Moshi amesema kuwa CPB imedhamiria kuwafikia wakulima wengi zaidi ili wazalishe kwa ufanisi shambani.

"Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) dhamira yake ni kuwawezesha wakulima kulima kwa kutumia mbinu za kisasa kwa maslahi yao binafsi na Taifa kwa ujumla,"ameeleza Dkt.Moshi

"Pia tunampango wa kuanza kutumia teknolojia ya kuzalisha mafuta ya kupikia yatokanayo na pumba za mpunga kupitia kiwanda chetu kilichopo Mkuyuni jijini Mwanza,"amesema Dkt.Moshi

Aidha,amesema kuwa kwa Mwaka 2021/2022 wamenunua mazao Tan Elfu 26,665 yenye Thamani ya shillingi Billion 14.8 na kuongeza Thamani mazao Tan elfu 16.3 yenye Thamani Billion 8.2.

Dkt. Moshi amesema kuwa ili mkulima apate mapato mengi anatakiwa kulima kwa Tija na kuendana na soko la kibiashara.

"Ikumbukwe kuwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), ni Taasisi ya serikali chini ya wizara ya Kilimo iliyopewa dhamana ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko na imeanzishwa kwa sheria ya nafaka na mazao changanyiko Namba 19 ambapo pia hadi sasa mzunguko wa biashara katika taasisi hiyo umeongezeka kutoka bilioni 15 hadi bilioni 52,"amesema Dkt.Moshi.

No comments:

Post a Comment