![]() |
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu Bi. Ruth Minja akitoa taarifa ya mwongozo wa uzinduzi huo utakavyofanyika wakati wa kikao hicho. |
![]() |
Mratibu wa Sensa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akitolea ufafanuzi baadhi ya taarifa zilizowasilishwa za maandalizi ya Uzinduzi huo. |
NA. MWANDISHI WETU - DODOMA
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya Oktoba 25, 2022 ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji inayohusisha Makatibu Wakuu Kwaajili ya Maandalizi ya Uzinduzi Wa Matokeo Ya Kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi Utakaofanyika Oktoba 31,2022 Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment