TANZANIA KUPITIA SHIRIKA LA POSTA INATARAJIA KUSAINI MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA SERIKALI YA CONGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 19, 2022

TANZANIA KUPITIA SHIRIKA LA POSTA INATARAJIA KUSAINI MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA SERIKALI YA CONGO


DRC, Congo

Tanzania kupitia Shirika lake la Posta inatarajia kusaini makubaliano ya kinoashara yanayolenga kuboresha bishara za mpakani (Cross boarder business) kupitia ziwa Tanganyika kutokea Kigoma kwenda DRC kupitia Kalemie jijini humo.

Hayo yameelezwa na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo wakati aliposhiriki Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji katika Sekta ya TEHAMA lililoanza jana tarehe 18 Oktoba, 2022, jijini Lubumbashi.

Wageni Rasmi katika Kongamano hilo ni Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeongoxana na Katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi na Mhe. Augustin Kibassa Maliba, Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akiwa katika Kongamano hilo, Postamasta mkuu ameeleza namna ambavyo Shirika la Posta nchini imejipanga kimkakati kushirikiana na Serikali ya DRC katika kuwahudumia wananchi wa Congo hususani kupitia Duka lake la Mtandao (E - Shop) linalowawezesha wananchi kuuza, kutangaza na kununua biidhaa mtandaoni mahali popote walipo.

Katika hatua nyingine Mbodo ameongeza kuwa, kutokana na fursa mbalimbali zilizopo Tanzania hasa kupitia Shirika la Posta nchini, Shirika la Posta linatarajia kusaini makubaliano ya mashirikiano katika maeneo mbalimbali ya kibiashara ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Posta katika nchi zote mbili

Kongamano hilo lenye zaidi ya washiriki 300 limehudhuriwa na Taasisi mbalimbali za Tanzania ikiwemo TAnTRADE, TTCL, Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki na TPSF.

No comments:

Post a Comment