VIJANA WATAKIWA KUONDOKANA NA IMANI POTOFU JUU YA CHANJO YA UVIKO-19 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 6, 2022

VIJANA WATAKIWA KUONDOKANA NA IMANI POTOFU JUU YA CHANJO YA UVIKO-19


Mratibu msaidizi wa chanjo Jiji la Dodoma Bi Frola Kimaro akizunguza leo Oktoba 6,2022 Jijini Dodoma wakati akifunga mafuzo kwa watendaji wa kata,Watendaji wa mitaa , viongozi wa dini na wataalam wa Afya na mafunzo yalikuwa ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko-19 - sambamba na kupata Chanjo ya Uviko - 19 yaliyoratibiwa na Shirika la Internews katika mradi wake wa Boresha Habari.
Sehemu ya washiriki wa mafuzo kwa watendaji wa kata,Watendaji wa mitaa , viongozi wa dini na wataalam wa Afya na mafunzo yalikuwa ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko-19 - sambamba na kupata Chanjo ya Uviko - 19 yaliyoratibiwa na Shirika la Internews katika mradi wake wa Boresha Habari.
Sehemu ya washiriki wa mafuzo kwa watendaji wa kata,Watendaji wa mitaa , viongozi wa dini na wataalam wa Afya na mafunzo yalikuwa ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko-19 - sambamba na kupata Chanjo ya Uviko - 19 yaliyoratibiwa na Shirika la Internews katika mradi wake wa Boresha Habari.

Na Okuly Julius-Dodoma

Imeelezwa kuwa kundi linalotakiwa kutiliwa mkazo katika uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa sasa ni kundi la Vijana kwani wamekuwa na imani potofu juu ya chanjo hizi kwamba wanaweza kukosa nguvu za kiume au kushindwa kuzaa kabisa mara watakapochanja.

Haya yamesemwa leo Oktoba 6,2022 Jijini Dodoma na Mratibu msaidizi wa chanjo Jiji la Dodoma Bi Frola Kimaro  wakati akifunga mafuzo kwa watendaji wa kata,Watendaji wa mitaa , viongozi wa dini na wataalam wa Afya na mafunzo yalikuwa ni kuwajengea uwezo wadau hao namna ya kutumia vyombo vya habari katika kuelimisha Jamii juu ya kujikinga na Uviko-19 - sambamba na kupata Chanjo ya Uviko - 19 yaliyoratibiwa na Shirika la Internews katika mradi wake wa Boresha Habari.

"Kundi la kuhamasisha sana kwasasa ni kundi la vijana kwani wamekuwa na imani potofu juu ya hizi chanjo kwa kusema wanaweza kosa nguvu za kiume au hata kutokuzaa kabisa".

Aidha Bi Frola amesema kuwa mwenendo wa utoaji wa chanjo kwa Jiji la Dodoma unaendelea na mpaka sasa kuna vituo vya Afya vinavyotoa huduma za chanjo 65 vikiwemo vituo vinavyotembea.

"Mwenendo wa utoaji wa chanjo kwa Jiji la Dodoma,tuna vituo 65 vya Afya vikiwemo vinavyotembea na vinaendelea kutoa huduma za chanjo wilaya ya Dodoma mjini".

Pia Mratibu huyo amesema mpaka sasa Tanzania bado hakuna mamlaka yeyote ya Afya iliyothibitisha kutokuwepo kwa ugonjwa wa Uviko19 hivyo watu waendelee kuchukua tahadhali kama kawaida.

"Kwa Tanzania bado hatujathibisha kuwa ugonjwa wa Uviko haupo,bado wataalamu hawajasema chochote hivyo tuendelee kuchukua tahadhali kama kunawa mikono na maji tiririka na sabuni,kuvaa barakoa na kuendelea kueluka mikusanyiko isiyo ya lazima".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo haya Shehe Musa Kalasa amesema yeye alichanja kwa utata sana kwani aliamini akichanja damu itaganda kama watu wanavyosema,lakini baada ya kupata elimu alichanja na hakupata shida yeyote.

Naye Bi Jane Shemndolwa Afisa mtendaji Halmashauri ya Mpwapwa kata ya Chitemo amesema alikuwa haamini kuhusu chanjo kutokana na maneno ya watu kuwa ukichanja chanjo ya Uviko19 unakuwa Zombi.

Juvenary Tailo aliyemwakilisha Mchungaji wa Kanisani MRB Prophetic Ministries amesema yeye alijua chanjo ni mpango wa kishetani wa kupunguza watu lakini baada ya kuhudhuria mafunzo haya amepata elimu na ameona mambo haya hayahusiani na chanjo.

Mafunzo haya yameandaliwa na  Internews Tanzania na kutolewa  na Wakufunzi ( Regional Trainers) Ndugu Bilson Vedastus na Fatuma Zahoro yamekusanya watu mbalimbali akiwemo Viongozi wa dini ili kupata uelewa wa pamoja na wao kwenda kutoa elimu kwa jamii zao.

No comments:

Post a Comment