WAZIRI MKUU AWASILI KOREA KUSINI KWA ZIARA YA KIKAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 24, 2022

WAZIRI MKUU AWASILI KOREA KUSINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea maua kutoka kwa watoto Neviah Mwamlima (kushoto) na Bradley Massawe wakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini Korea ya Kusini, Oktoba 24, 2022 kuanza ziara ya kikazi nchini humo. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Togolani Mavura.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini, Mhe. Togolani Mavura wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon nchini Korea ya Kusini Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi nchini humo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim. Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakisalimiana na baadhi ya watanzania waishio nchini Korea ya Kusini waakati walipowasili kwenye hoteli ya Lotte iliyopo Seoul nchini humo Oktoba 24, 2022 kwa ziara ya kikazi .

*********************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumatatu, Oktoba 24, 2022) amewasili Seoul, Jamhuri ya Korea Kusini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Mheshimiwa Majaliwa alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Togolani Mavura pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika nchi hiyo.

Kesho (Jumanne, Oktoba 25, 2022) Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea kkampuni ya kutengeneza mabehewa na injini za treni cha SRT kilichopo katika mji wa viwanda wa Mungyeong pamoja na kituo cha ubunifu kilichopo Pangyo. 

Aidha, akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini. 

Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.

No comments:

Post a Comment