Na WAF- DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya yaja na mpango wa kusomesha Watumishi wa afya katika fani ya ubingwa na ubingwa bobezi, ambapo mafunzo hayo yatatolewa kwa set, huku jumla ya Watumishi 139 wamechaguliwa kupata ufadhili wa masomo hayo, huku kati ya hao, Watumishi 136 watasomeshwa nje ya nchi na Watumishi 3 watasomeshwa ndani ya nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Oktoba 28, 2022 wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Serikali wa kuendeleza Watumishi wa Sekta ya Afya katika fani za ubingwa na ubingwa bobezi nchini.
Waziri ummy amesema, Mpango umepewa jina la "Mpango wa Samia wa kuongeza Wataalamu Bingwa na Bobezi wa Afya nchini " utakao gharimu shilingi Bilioni 8.
Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali kuongeza fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 8 zitakazotumika kugharamia wataalamu waliochaguliwa kusoma mafunzo haya.
No comments:
Post a Comment