MIRADI YA KIMKAKATI INAYOTEKELEZWA HAPA NCHINI NI DARASA TOSHA KWA WAHANDISI WAZAWA-ERB - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 10, 2022

MIRADI YA KIMKAKATI INAYOTEKELEZWA HAPA NCHINI NI DARASA TOSHA KWA WAHANDISI WAZAWA-ERB

Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2022 Jijini Dodoma ( hawapo pichani) ,wakati akielezea shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023.
Baadhi ya Waandishi wa Habari, wakimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe,wakati akielezea shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023, leo Novemba 10,2022 Jijini Dodoma
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa (Wa kwanza kushoto) na Baadhi ya Waandishi wa Habari, wakimsikiliza Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe,wakati akielezea shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023, leo Novemba 10,2022 Jijini Dodoma


Na Okuly Julius-Dodoma

BODI ya Wahandisi nchini (ERB) ,imesema kuwa uwepo wa Miradi mikubwa ya Kimkakati inayotekelezwa hapa nchini imekuwa manufaa kwa Wahandisi wazawa hasa vijana kupata ujuzi kwani miradi hiyo iliyokuja na Teknolojia mpya.

Mifano ya miradi hiyo ya Kimkakati inayoendelea ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya kisasa ya Mwendokasi (SGR) na ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo imekuwa kama darasa kwa vijana wa kitanzania wanoshiriki katika ujenzi wa Miradi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10,2022 Jijini Dodoma, Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Bernard Kavishe ,wakati akielezea shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023, amesema kuwa miradi hiyo imekuja na teknojia mpya kabisa.

Ambapo Mhandisi Kavishe amesema kuwa ,kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya Wahandisi 33,773, kati yao 26,000 wapo katika soko la ajiri huku wenye leseni za Uhandisi wakiwa ni 10,000 na wengi wao wanashiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa inayoendelea.

"Tanzania tunakadiriwa kuwa na jumla ya Wahandisi 33,773 kati yao 26,000 wapo Sokoni na kati ya hao wenye leseni za Uhandisi wakiwa ni 10,0000 tu ,

Na kuongeza kuwa" Tuna Mafundi sanifu 1,979 na maabara za kihandisi 40 si mnajua mnapotaka kujenga ni lazima eneo lipimwa na iangaliwe pia kwa eneo unalotaka kujenga ni aina gani au ni muundo gani inayostahili kutoakana na mazingira kwa ujumla hapo ndio kazi ya maabara zetu zinaanzia,"Amesema Mhandisi Kavishe


Mhandisi Kavishe amesema kuwa Bodi hiyo imeshasajili Makampuni 398 inayojishuhulisha na masuala ya uhandisi huku makapuni 275 kati ya hayo ni ya ndani ya nchi wakati makampuni 123 yakiwa ni kutoka nje ya nchi.

Aidha, Mhandisi Kavishe amebainisha kuwa malengo ya Bodi hiyo ni kuongeza ushiriki wa bidhaa za ndani (Local content) katika miradi yote inayoendelea hapa nchini.

"Tutaongeza ushiriki wa bidhaa za ndani katika utekelezaji wa miradi inayoendelea kwa mfano kwa sasa Saruji yote inayotumika katika ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere inazalishwa hapa nchini hivyo malengo ya bodi ni kuona vifaa vyote vinatoka hapa nchini hiyo pia itasaidia sana kuongezea nchi mapato maana watu watauza serikali itapata kodi yake,"Amebainisha Mhandisi Kavishe

Mhandisi Kavishe amesema kuwa Matarajio makubwa ya Bodi hiyo ni kujenga kituo Cha Umahiri Jijini Dodoma,kutokana na kuwepo kwa Vijana wengi wenye mawazo ya kibunifu ila wanakosa namna ya kuendeleza mpaka kufika sokoni ,hivyo kituo hicho kitakuwa eneo sahihi la kuendeleza mawazo hayo.

"Kuna vijana wengi wenye mawazo mazuri kabisa ila namna ya kuendeleza inawawia vigumu sana ila tumeona sisi kama bodi suluhisho lake ni kujenga kituo cha umahiri ambapo itatumika kuendeleza vijana na Itakuwa na maabara pia," Amesema Mhandisi Kavishe

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kuwa kwa sasa nchi ina miradi mingi hivyo nafasi ya Bodi ya Wahandisi ina nafasi kubwa katika kutoa ushauri namna gani nzuri ya kutekeleza miradi hiyo kwa uhakika.

"Nafasi ya ERB ni kubwa sana katika maendeleo ya Taifa letu kwani kila penye Mradi unaoendelea ERB wapo na wanathibiti ubora wa kazi na wa Mhandisi anayejenga ule mradi hivyo niwaambieni tu hii ni bodi kongwe na haya majengo mnayoyaona yote kuna Mkono wa ERB,"Amesema Msigwa

Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Imeanzishwa Mwaka 1968, ikiwa na majukumu ya Kusajili Wahandisi,kuendeleza wahandisi na kutoa hithibati kwa waandisi , hayo majukumu yote ERB inayatekeleza kwa ajili ya usalama wa nchi na kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

No comments:

Post a Comment