Na Mwandishi wetu Dodoma
Mkoa wa Dododma umepokea kiasi cha Tsh.6,780,000,000/- kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339, katika shule 127, zilizopo katika halmashauri 8 za Mkoa huo.
Miongoni mwa shule ambazo mkuu wa mkoa ametembelea katika ziara hiyo ni shule ya sekondari Viwandani na shule ya sekondari Zuzu. Shule hizi zote zinaendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo kila moja inajenga madarasa mawil. Madarasa hayo yamefikia hatua ya kuezeka na kumalizia hatua za mwisho.
Akiwa shule ya sekondari Zuzu, Mkuu wa Mkoa amewataka wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kusimamia mradi huo ili umalizike kwa wakati.
“Hakikisheni mnamaliza lakini kwa uzuri, ubora na uharaka, hakikisheni mnamalizi mradi kwa wakati. Rais ametoa fedha shilingi Bilioni 6.780 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 339 kwenye shule mbalimbali za mkoa wa Dodoma. Tuna jukumu la kusimamia fedha hizi zitumike ipasavyo” RC Senyamule
Akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa shule hiyo Bw. Hezron Lupondo, amesema shule ilipokea shilingi Milioni 20 kwenye akaunti ya shule kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo.
“Mradi ulianza Oktoba 10 na mpaka sasa umefikia hatua ya upauaji, kuweka kenchi, plasta, madirisha na milango. Tunatarajia mpaka Novemba 20 mradi utakua umekamilika” Amesema Bw. Lupondo
Mbali na ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ametoa rambirambi za Serikali ya Mkoa kwa Familia ya Marehemu Neema Faraja Samwel ambaye alikua mwenyeji wa Dodoma na mfanyakazi wa Shirika la MDH, aliyepoteza maisha kwenye ajali ya ndege iliyotokea mkoani Kagera Novemba 6.
" Natoa pole kwa familia ya Neema, mshikeni sana Mungu wakati huu pia natoa pole kwa Shirika la MDH kwa kupoteza wenzao kwani tunajua shirika hili linafanya kazi kwa karibu na Serikali. Serikali imeshiriki msiba huu kuanzia Kagera tulipowakilishwa na Mhe. Waziri Mkuu. Serikali imeguswa sana kwani ni tukio lililotushtua na Serikali inaendelea kuchunguza chanzo cha ajali. Serikali ya Mkoa inatoa rambirambi ya Shilingi Milioni moja na tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na familia katika kila hatua” Amesema Mhe. Senyamule
No comments:
Post a Comment