WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUPIGA VITA UKATILI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 21, 2022

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUPIGA VITA UKATILI.


Na Renatha Msungu -Dar es Salaam

WAANDISHI wa Habari Wanawake kutoka Vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini,wamepatiwa mafunzo kuhusu kuzuia ukatili wa kijinsia katika soka la wanawake.

Semina hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa Global Foundation na Mkufunzi Idd Mziray na Katibu wa chama cha soka cha wanawake TWFA.


Idd Mziray amesema lengo la mafunzo hayo kwa waandishi ni pamoja na kwenda kutumia kalamu zao kwa ajili ya kupiga Vita ukatili kwenye soka la wanawake.

Mziray amesema waandishi ni kioo cha jamii hivyo kalamu zao zikitumika vizuri zitasaidia kupunguza au kutokomeza ukatili katika soka la wanawake.


"Naomba waandishi mkawe mstari wa mbele kupiga vita suala la ukatili katika soka la wanawake,"alisema Mziray.

Naye katibu wa TWFA somoe Ng'itu amesema soka la wanawake limepelekwa juu na waandishi wa habari hivyo kizazi kinachochipukia kizidi kuliandika ili jamii ielewe.

"Naomba waandishi muendelee kulipigia kelele soka la wanawake ili litambulike, "alisema Somoe.


Somoe amesema semina hii ikawe chachu ya kuchochea soka la wanawake ili liweze kusonga mbele kama ilivyo katika nchi nyingine.

Amesema kuwajengea uwezo waandishi katika kuunga mkono juhudi za kuondoa mitazamo hasi iliyopo katika jamii kuhusu soka la wanawake kwa kutoa elimu stahiki kutasaidia kiasi kikubwa kuutokomeza.

Amesema elimu hiyo ukatolewe kila mahali ili kuhakikisha soka la wanawake linaemlndelea kukua bila kuwepo na ukatili wowote kwa wachezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa GPF TZ Martha Nghambi amewashukuru waandishi wa habari huku akiwataka kwenda kutumia kalamu zao kupiga vita ukatili kwenye soka la wanawake.

No comments:

Post a Comment