BABA MTAKATIFU MSTAAFU BENEDIKTO XVI AFARIKI DUNIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 31, 2022

BABA MTAKATIFU MSTAAFU BENEDIKTO XVI AFARIKI DUNIA


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Jumatano tarehe 28 Desemba 2022 kuhusu Sherehe ya Noeli, Mwaliko kwa waamini kutafakari pamoja na Wasalesian wa Don Bosco, Mama Kanisa anapoanza kuadhimisha Jubilei ya Miaka 400 tangu Mtakatifu Francisko wa Sales, Askofu, Mwalimu wa Kanisa na Msimamizi wa Waandishi wa Habari alipofariki dunia tarehe 28 Desemba 1622, aliwaalika kwa namna ya pekee kabisa, waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kumwombea Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ambaye alikuwa mgonjwa sana.

Tarehe 16 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliadhimisha Kumbukizi ya Miaka 95 tangu alipozaliwa.

Tangu mwaka 2013 amekuwa akiishi kwenye Hosteli Mater Ecclesiae iliyoko ndani ya Bustani za Vatican. Haya ni maisha yanayosimikwa katika sala, tafakari ya Neno la Mungu, Muziki pamoja na kujisomea binafsi.

No comments:

Post a Comment