MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU WAMEFANYIWA VIPIMO VYA AFYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, December 11, 2022

MADEREVA WA MALORI YA MASAFA MAREFU WAMEFANYIWA VIPIMO VYA AFYA


Na Renatha Msungu -Dar-es-salaam 

MADEREVA wa malori ya masafa marefu wamefanyiwa vipimo vya Afya kwa ajili ya kujua afya zao ili kuepusha ajali mbalimbali zinazotokea Barabarani katika maeneo mbalimbali.

Zoezi la upimaji afya za madereva zimefanyika katika kongamano lililoandaliwa na North Star Alliance jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kongamano hilo Meneja mradi kutoka North Star Alliance Steve Mhando alisema wameamua kufanya hivyo ili kuepusha madereva kunywa dawa hovyo bila kupima kujua wanatatizo gani la afya.

"Kongamabo kama hili hufanyika kila mwaka na hii ni kuondoa mazoea yakunywa dawa bila kwenda hospital, "alisema Mhando.

Hata hivyo amewaasa madereva kujenga utaratibu wa kwenda hospital kucheki afya zao kabla ya kuanza safari za masafa ya mbali.

Alisema wameshafanya zoezi hilo kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wanafanikiwa.

Alisema lengo lao ni kuona madereva wanakuwa fiti kwa sababu sehemu kubwa ya maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuangaliwa.

Alisema baada ya kufanya utafiti ilionekana madereva wanahitaji sana Huduma za afya badala ya kununua madawa.

Alisema baada ya kushirikiana na serikali kutengeneza vituo hivyo ambavyo vingi vipo Barabarani kwa ajili ya kuwasaidia madereva wakiwa safarini.

Alisema kongamano hilo litaendelea kufanyika kila mwaka na hii ni kuwasaidia madereva wanaoenda masafa marefu na vyombo vya moto.

Hata hivyo ameishkuru serikali kutokana na ushirikiano wanaofanya katika utekelezaji wa kongamano hilo kila mwaka hapa nchini.

No comments:

Post a Comment