MAFUNZO KWA WAVUVI YAENDELEA VISIWANI MKOANI KAGERA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 2, 2022

MAFUNZO KWA WAVUVI YAENDELEA VISIWANI MKOANI KAGERA


Na Mwandishi wetu Kagera 

Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo Cha maafa imeendelea kutoa Mafunzo ya kuimarisha ujuzi wa uokoaji kwa vikundi vya maokozi vya wavuvi wa kisiwa cha Gozba na bumbile Mkoani Kagera ikiwa Ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya waziri mkuu aliyoitoa Novemba 7 katika uwanja wa Kaitaba wakati wa kuaga miili ya marehemu 19 waliokufa katika ajali ya ndege.


Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya waziri mkuu, Luten Kanali Selestine Masalamado amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha ajali na maafa zinapungua au kuisha kabisa ikiwa ni pamoja na kuokoa maisha ya watu na kupunguza upotevu wa mali wakati wa ajali katika upande wa Bahari na Maziwa kuu.


Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Ndugu Toba Nguvila ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuleta mafunzo kwa wavuvi hao na amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndugu Elias Kayandabila kutengeneza namna ya kuendelea kutoa mafunzo kwa wavuvi wengine ili elimu izidi kuwafikia wengi na kumaliza maafa ya majini.

No comments:

Post a Comment