TAMBO ZA MASHABIKI WA KAGERA SUGAR KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA SIMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 21, 2022

TAMBO ZA MASHABIKI WA KAGERA SUGAR KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA SIMBA


Na Gideon Gregory, Kagera.

Mashabiki wa timu za soka za Kagera Sugar na Simba wamejinasibu kuibuka na ushindi katika mtanange wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara utakao chezwa majira ya saa 07:00 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ulioko mkoani Kagera.

Wakizungumza na OKULY BLOG  kwa nyakati tofauti wametanabaisha kuwa wana imani na vikosi vyao kutokana na jinsi walimu wa timu zote mbili walivyo andaa timu hizo.


Kwa upande wao Kagera Sugar wamesema wamejipanga vilivyo kuibuka na ushindi licha ya mchezo wa mwisho kutoa sare dhidi ya wana ramba ramba wa Azam FC ya kufungana mabao 2-2 hivyo haiwavunji na ikichagizwa wako na mwalimu mpya Mecky Maxime.

“Hawa Simba hatuna wasiwasi nao maana tumewafuatilia kwa ukaribu katika michezo yao waliyo cheza hivi karibuni kwahiyo tunawamuda vizuri,”wamesema.


Nao Simba wamesema wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wao wana kikosi bora kuzidi wapinzani wao hivyo hawaogopi na watahakikisha wanaondoka na alama zote tatu hii leo.

“ Ukiangalia kwa sasa wanacheza kitimu na kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo wa leo na kumbuka tunakimbizana na kinara wa ligi ambaye ni Young Africans kwahiyo leo ushindi ni lazima,”wamesema.

Ikumbukwe kuwa mchezo wa mwisho waliocheza katika uwanja huo Simba walipoteza kwa kufungwa goli 1-0 mchezo uliopigwa Januari 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment