![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda akizungumza na wanahabari wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania juu ya utekelezaji wa mpango wa mbolea za ruzuku kwa wananchi wa wilaya hiyo. |
![]() |
Mkulima Tatu Ramadhani mnufaika wa mbolea za ruzuku aking'olea majani kwenye shamba lake la mahindi lenye ukubwa wa ekari 2 |
Na Mwandishi wetu Singida
Imeelezwa kwamba, Wilaya ya Iramba mkoani Singida ni miongoni mwa wilaya zilizonufaika na mpango wa serikali wa kutoa mbolea za ruzuku ambapo mpaka tarehe 5 Desemba, 2022 zaidi ya tani 600 za mbolea sawa na Mifuko 12360 yenye thamani ya shilingi bilioni 1 na milioni 500 zimewafikia wakulima wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yusuph Mwenda amesema, kwa mwaka 2021 wakulima walinunua mbolea mpaka kiasi cha shilingi 135,000 kwa mfuko mmoja ambapo si wote waliomudu gharama hiyo na hivyo kupelekea kupungua kwa uzalishaji kwani baadhi yao walipunguza ukubwa wa mashamba waliyolima na wengine hawakulima kabisa.
Mwenda amesema hayo hivi karibuni alipofanya mahojiano na wanahabari kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) waliofika ofisini kwake kwa lengo la kufanya tathmini ya mwitikio wa wakulima kwenye matumizi ya mbolea pamoja na kuandaa makala inayoangazia manufaa yatokanayo na mpango wa mbolea za ruzuku kwa wakulima msimu wa kilimo 2022/2023.
Mwenda alisema Wilaya kwa niaba ya serikali inasimamia
mipango na mikakati iliyowekwa na serikali na chama katika kuhakikisha kilimo kinaongeza tija na wakulima wanajihusisha na kilimo biashara kwa kupata pembejeo zote ikiwemo mbolea.
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya Mwenda alisema takribani kata 10 hadi 12 kati ya kata 20 za wilaya hiyo zinajihusisha na ¹kilimo cha mbolea za windani na kubainisha kuwa kufuatia hamasa na uwepo wa mbolea za ruzuku kwa mwaka 2022 mahitaji ya mbolea wilayani humo yameongezeka.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo katika Halmashauri ya Iramba, Marieta Kasongo alisema Wilaya inajumla ya kaya 45000 zinazojihusisha na kilimo na kueleza kuwa mpaka sasa wamesajili wakulima 17,064na usajili unaendelea.
Aliongeza kuwa awali mwitikio wa wakulima kujisajili ulikuwa mdogo mpaka pale walipoona mbolea zimefika wakulima waliojiandikisha pekee ndio walioweza kununua mbolea hizo kwa bei ya ruzuku.
Kwa upande wake mkulima Yusuph Kingu,alishukuru utaratibu uliowekwa na viongozi wao wa kilimo katika kuhakikisha wanajisajili na kuwapa namba zinazowawezesha kununua mbolea kwa bei ya ruzuku na kwa wakati.
Aidha, aliwashauri wakulima wa Iramba wanaopenda kuamini baada ya kuona kuwa wanachelewa kunufaika na kuwataka kufuata maelekezo ya serikali ili waweze kunufaika na mpango wa ruzuku za mbolea uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan
No comments:
Post a Comment