WANAFUNZI TANZANIA NA CHINA KUBADILISHANA UZOEFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 1, 2022

WANAFUNZI TANZANIA NA CHINA KUBADILISHANA UZOEFU


Na WyEST,DSM

# Mkataba ushirikiano wasainiwa DIT na Taasisi ya Ufundi (CQVIE) ya China

# Prof. Mkenda ashuhudia utiaji saini  makubaliano

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshuhudia utiaji  saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Taasisi ya Ufundi ya Chonqing (CQVIE) kutoka nchini China.

Waziri Mkenda amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka Tanzania ikiwa katika mchakato wa MAGEUZI makubwa katika elimu.

Miongoni mwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo ni kubadilishana Wanafunzi na Walimu (exchange program ) ili kubadilishana uzoefu katika ujuzi wanaopata katika mafunzo.


Pia wanafunzi wanufaika wa programu hiyo watakuwa na sifa za kufanya kazi katika makampuni mbalimbali nchini China.

Prof. Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha ushirikiano huo unadumu na unakuwa endelevu kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment