Na. Majid Abdulkarim, WAF- KATAVI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kasim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Afya kwa kutekeleza maagizo ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi ambapo kwa sasa imefikia asilimia 92 kwa Wing A kutoka asilimia 40 mwaka jana.
Mhe Majaliwa ametoa pongezi hizo leo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo amekuta kunaongeza la kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kutekelezwa maagizo yake ya kushirikiana na ofisi ya Mkoa katika kusimamia mradi huo, Maagizo hayo aliyatoa mwaka jana 2021 mwezi wa nane.
Awali Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof Abel Makubi alitoa taarifa kuwa mradi wa Wing A utakamilika tareh 31 Disemba 2022 na huduma zitaanza kutorea tarehe 01 Januari 2023 na Ujenzi wa Wing B unategemea kukamilika Oktoba 2023.
Mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa sasa umetumia kiasi cha shilingi bilioni 9 .2 zilizotolewa na serikali kati ya bilioni 12.3 , ameeleza Prof. Makubi
Prof Abel Makubi amesema Hospital zote za Rufaa za Mikoa nchi nzima zitapatiwa mashine za CT Scan kwa ajili ya kutoa huduma ya uchunguzi kwa wananchi.Pia ameeleza kuwa Hospitaal ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kulaza Wagonjwa 170 kwa wakati mmoja.
Mheshimiwa Waziri Mkuu yuko mkoani Katavi kwa ziara ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment