Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Dkt. Selemani Jafo, ameshiriki vikao mbalimbali vya kubadilishana mawazo katika masuala ya biashara ya hewa ya ukaa Dubai.
Ziara yake ya kikazi imeanzia katika Ofisi ya Ubalozi mdogo uliopo Dubai na kukutana na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Balozi Iddi Seif Bakari.
Pia Dkt. Jafo amekutana na kufanya kikao na viongozi na watendaji wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON ya Dubai.
Ziara hiyo ya kikazi ni mwendelezo wa maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiunchumi.
Serikali ya Dkt. Samia kwasasa inaifungua Tanzania katika nyanja pana ya mazingira duniani kwa kupitia biashara ya hewa ya ukaa baada ya Tanzania kuweka muongozo na kanuni za biashara ya Hewa ya Ukaa ambayo inatarajiwa kuongeza pato la Taifa kwa siku chache za usoni na kuiweka Tanzania katika sura nzuri ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kimazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
No comments:
Post a Comment