MHAGAMA AWEKA WAZI TAASISI ZINAZOONGOZA KWA UVUNJIFU WA MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 30, 2023

MHAGAMA AWEKA WAZI TAASISI ZINAZOONGOZA KWA UVUNJIFU WA MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe.Jenista Mhagama akizungumza  Leo Januari 30,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kilichojadili matokeo ya utafiti wa uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma mwaka 2022.


Na Okuly Julius, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe.Jenista Mhagama amesema taasisi za Polisi,Mahakama,Manunuzi ya  Umma,Mikataba na Usimamizi wa Ardhi zinaongoza kwa viashiria vya uvunjifu wa maadili katika utumishi wa umma.

Pia amesema kiwango cha uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma kwa mwaka huu kimeongezeka hadi kufikia asilimia 75.9 ikilinganishwa na uliofanyika mwaka 2014 ambao kiwango kilikuwa asilimia 66.1.


Jenista ameeleza hayo jijini Dodoma Leo Januari 30,2023 akifungua kikao kazi cha usimamizi wa maadili katika utumishi wa umma kilichojadili matokeo ya utafiti wa uzingatiaji wa maadili katika utumishi wa umma mwaka 2022.

"Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kuna baadhi ya maeneo badomkuna shida mfano taasisi za Polisi,Mahakama,Manunuzi ya Umma,Mikataba na Usimamizi wa Ardhi huko bado kunahitajika ufuatiliaji mkubwa kwa sababu ni maeneo yanayoongoza kwa viashiria vya ufunjifu wa maadili katika utumishi wa umma,"amesema Mhagama

Mhagama  amewaagiza wajumbe wa kikao hicho kuhakikisha wanaangalia kwanini taasisi hizo zinaendelea kuongoza na nini kifanyike ili kuondokana na changamoto hiyo.


"Kufanya utafiti ni kazi moja na kutoa matokeo ya utafiti ni Jambo lingine, hivyo hakikisheni unapokea taarifa,mkayabaini yaliyoko kwenye tafiti hizo na kuyafanyia kazi,"amesema

KUHUSU ONGEZEKO LA MATOKEO

Waziri Mhagama amesema kuongezeka kwa matokeo hayo kunatokana na jitihada za kuimarisha uzingatiaji wa maadili chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.


”Matokeo ya utafiti huu yanaonesha juhudi za serikali za kuchukua hatua mbalimbali za kuweka misingi imara ya usimamizi wa maadili, kuweka mazingira wezeshi na kuimarisha uwajibikaji katika utumishi wa umma,"alisema Waziri Jenista.

Pia amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, kufanya kikao kazi cha pamoja na wadau kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kina kuhusu matokeo ya utafiti huu na kuja na mikakati ya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa maadili katika sekta zote kulingana na matokeo.

Katika hatua nyingine aliwataka Waajiri kuhakikisha wanatenga bajeti ya mafunzo ya maadili na kuendesha mafunzo kwa watumishi wa umma walio kazini na wale wanaoajiriwa.


Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mipango kutoka ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Cosmas Ngangaji amesema wakisimamia utumishi wa umma Kwa kutumia Sera, mifuko na usimamizi wa rasilimali watu katika Utumishi wa umma, watafikia malengo na matarajio ya Serikali na utaratibu huo  lazima ushuke mpaka ngazi ya familia.

No comments:

Post a Comment