TANZANIA YAKABILIWA NA KASI KUBWA YA UKUAJI WA MIJI NA VIJIJI-RIDHIWANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 17, 2023

TANZANIA YAKABILIWA NA KASI KUBWA YA UKUAJI WA MIJI NA VIJIJI-RIDHIWANI


Na Gideon Gregory, Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zinakabiliwa na kasi kubwa ya ukuaji wa Miji na Vijiji kutokana na ongezeko kubwa la watu jambo linalochagizwa na kushamiri kwa maendeleo nchini.

Naibu Waziri Kikwete, ameyasema hayo leo Januari 17,2023 Mtumba Jijini Dodoma katika mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP), akimwalisha Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Mh. Dkt. Angelina Mabula uliokuwa na kauli mbiu isemayo “Uboreshaji milki wa maendeleo endelevu”.

“Ongezeko hili la watu kwa hoja nyingine limekuja kutokana na madiriko katika maeneo mbalimbali mfano ongezeko hili limechagiza ukuaji wa miji yetu lakini pia mabadiriko ya vijiji vyetu sasa kuwa miji,”amesema.

Amesema mradi huo utagarimu jumla ya Dola za Kimerekani Milioni mia moja hamsini ($150,000,000) sawa na takribani Shillingi za Kitanzania bilioni 345, ambapo umepangwa kutekelezwa kwa muda wa miaka mitano (5) kuanzia Mwezi Julai, 2022 hadi mwezi Juni, 2027 katika mikoa 16 ya Pwani, Simiyu, Iringa, Tanga, Tabora, Geita, Kigoma, Mara, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Kilimanjaro, Ruvuma, Songwe, Katavi na hivi karibuni Mkoa wa Arusha zenye jumla ya halmashauri 41.

“Mradi huu ni wa kwanza kwa ukubwa katika sekta ya ardhi kuwezeshwa na Benki ya Dunia Kusini kwa nchi za chini ya Jangwa la Sahara, mradi huu wa LTIP utatumiwa na Benki ya Dunia kupima

sio tu uwezo wa watanzania kusimamia na kutekeleza miradi mikubwa katika sekta ya Ardhi kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla bali pia utatumika kupima uwezo wa nchi za Afrika katika kutekeleza miradi mikubwa kwenye Sekta ya Ardhi,”amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi amesema tarehe 21 Januari 2022, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilisaini mkataba na Benki ya Dunia wa Shilingi 346 bilioni (USD 150 milioni) kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Kuboresha Usalama wa Miliki za Ardhi nchini.

Amesema Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, ilianza maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo ambapo kulingana na makubaliano vimeundwa vyombo vya usimamizi wa utekelezaji na uratibu ambavyo ni Kamati ya Uongozi inayojumuisha makatibu Wakuu wa Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha na TAMISEMI, Kamati ya Ufundi ya (Project Technical Committee) inayojumuisha wakuu wa Idara, vitengo na Sehemu zenye kazi katika mradi na wawakilishi kutoka Wizara ya fedha na OR-TAMISEMI.

“Timu ya Kuratibu Utekelezaji wa Mradi (Project Implementation Team) inayojumuisha wataalam walioteuliwa na wataalam waelekezi walioajiriwa na serikali kwa Mkataba kusimamia maeneo ya usimamizi wa fedha, ugavi, tathmini na ufuatiliaji na masula ya kimazingira na kijamii na mkutano wa wadau ngazi ya taifa na ngazi za chini kwenye maeneo ya utekelezaji wa mradi,”amesema.

Naye mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Nicholas Meitiak Ole Soikan amesema wao kama Benki ya Dunia wanauangalia mradi huo na ameomba wawapatie uongozi wa njia ya kufanya mabadiriko katika sekta ya Ardhi.

No comments:

Post a Comment