OR-TAMISEMI, Morogoro
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amewataka vijana wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kutumia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri zote nchini kujiimarisha na kujijenga kimtaji.
Mhe. Kairuki ameyasema hayo kwenye Kongamano la University Ladies and Gentleman lililofanyika katika Chuo Cha Kilimo Cha SUA mkoani Morogoro tarehe 28.01.2023.
Amesema Serikali kupitia halmashauri imekuwa ikitoa mikopo asilimia 10 kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na kuwataka kutumia fursa hiyo kujijenga kiuchumi.
" Tuendelee kuzitumia fursa kama hizi kujijenga kiuchumi na pia kuongeza mitaji yenu ili muweze kukua na hatimaye kugraduate kutoka kwenye mikopo hiyo ambayo ni mahusi kwa wanaoanza biashara na wakikua huweza kwenda kwenye taasisi nyingine za fedha."
Kairuki amesema katika kipindi cha kati ya Julai hadi Desemba 2022 halmashauri zote nchini zimetoa Sh billion 28 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Pia amewasisitizia kutumia fursa hizo katika upatikanaji wa mitaji na fursa zingine zilizopo katika kilimo, ufugaji na uvuvi.
Amesema Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa elimu ya juu na kwa miaka 3 imetoa Sh trilioni 1.68 na kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza kwa kuongeza mikopo hiyo mwaka had mwaka.
" Niwapongeze wale walioamuwa kujiongeza na kuwa wathubutu na kuanza ujasiriamali wakiwa bado wanafunzi wa chuo hii itawasaidia kujiandaa na maisha pindi watakapo maliza masomo yao kwa sababu watakuwa tayar wameshaanzisha shughuli zao za kiuchumi.
Pia Mhe. Kairuki amesema kuna fursa za mikopo inayotolewa na Nssf kwa wajasiriamali wadogo wa viwanda kwa Kushirikiana na Benki ya Azania, Sido pamoja na Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi(NEEC) hivyo rai yangu kwenu zitumieni hizo fursa, jifunzeni kwa waliofanikiwa ili muweze kunufaika na fursa hizi kwa sababu Taifa letu linazidi kukua siku hadi siku na Serikali yetu haiwezi kuajiri watu wote wala Sekta binafsi hivyo ni vyema kuangalia na namna mnavyowezw kujiajiri.
Kwenye eneo hili pia ipo Taasisi au Programu ijulikanayo kama Jukwaa la Kizazi chenye Usawa ni jukwaa ambalo nchi zote duniani wameweza kujiunga nalo na Tanzania tumejiunga na kipengele cha Uwezeshaji wa Wananwake Kiuchumi na Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa kinara Duniani katika eneo hilo hivyo kupitia programu hii pia tutaona namna tunavyoweza kuwezesha wanawake vijana.
Mhe. Kairuki amesema “ Ni imani yangu kupitia kongamano hilo mtaendelea kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali yanayowahusu na sisi tutaendelea kuwashika mkono na kuhakikisha kwamba Taasisi hii inaendelea kukuwa na kuendelea kwenye kujenga uwezo wa vijana wa vyuo.
Kongamano hili limeandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Ladies Talk Tanzania Initiatives ambayo inajishughulisha na shughuli mbalimbali za vijana wa kike kwa lengo la kukuza na kuwainua kiuchumi kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali, elimu ya kijinsia, kujitambua, uongozi na uthubutu wa kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment