BMH YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 6, 2023

BMH YAANZA KUTOA HUDUMA ZA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO.


Na Okuly Julius-Dodoma

HOSPITAL ya Benjamin Mkapa imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za Upasuaji wa Moyo kwa watoto na Shirika lisilo la kiserikali la Children Heart Charity Association la nchini Kuwait.

Awali Hospitali ya Benjamin Mkapa ilikuwa inatibu watoto 400 kwa mwezi hivi sasa watakuwa na uwezo wa kutibu watoto 3400.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa DK Alphonce Chandika amesema makubaliano hayo yameangazia maeneo makuu matatu.


Ameyataja maeneo hayo kuwa ni kugharamia watoto wenye matatizo yanayohitaji Upasuaji wa moyo,kuwezesha vifaa tiba vinavyohitajika kwenye matibabu ya moyo.

Amesema eneo la tatu ni kuwajengea uwezo madaktari,wauguzi na wataalam wa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya Moyo wa Hospital ya Benjamin Mkapa.

"Tunaishkuru sana Kuwait kwa kujitolea kutusaidia matibabu ya Moyo kwa watoto wadogo,"amesema Dk Chandika.


Amefafanua zaidi ya kuwa pamoja na utiaji saini tayari jopo la Madaktari, wauguzi na wataalam wa huduma za matibabu ya Moyo kutoka Kuwait wamewasili katika hospital hiyo kutoa huduma za uchunguzi tokea February 3 ambapo watakuwepo hadi February 9 na wanatarajia kuwafanyia uchunguzi watoto 100 na kupatiwa matibabu.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Said Musa amesema ujio wa madaktari hao bingwa hapa nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za moyo kwa watoto ikiwemo Upasuaji.

Amesema anaishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kutokana na ushirikiano waliotoa kwa madaktari hao na kuwataka waendelee kuwa na Moyo wa utoaji matibabu ya Moyo.

Kwa upande wake Dr Faisal Al-Saied amesema wanaimani malengo wanayotarajia kuyafikia yatafanikiwa kwa sababu wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa Benjamin Mkapa.

Amesema jamii inapaswa ijitokeze kwa ajili ya kupata matibabu ya Moyo kwa watoto wadogo hususani wale wanaohitaji Upasuaji.

Mpaka sasa watoto wawili waliokuwa na tatizo la moyo wamefanyiwa upasuaji tangu ujio wa jopo hilo la wataalamu kutoka nchini Kuwait kufika katika hospitali ya Benjamin Mkapa.

No comments:

Post a Comment