Na Okuly Julius-Dodoma
"Utaratibu Huo Utasaidia kujua mienendo ya Magari Yote yanayopita Katika Barabara Kuu, Tutaanza Na Ya Kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma Hatua Kwa Hatua Ili Kila gari inayopita Katika Barabara hiyo popote ilipo, Tuweze kuiona Askari akiwepo Kwenye Control Center Makao Makuu"
Masauni Ameyasema hayo Leo February 10,2023 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Katika Jengo la Kambarage Tower.
Amesema Kuanzia Leo Wanataka Kufanya uhakiki Wa madereva Wote Nchini Hususani Wa Mabasi Na Malori Ili madereva Wote wanaoendesha Mabasi Ya Abiria wasajiliwe kwenye mifumo ya Data na Yeyote ambaye atakuwa hajasajiliwa hataruhusiwa Kuendesha Gari.
Waziri huyo Ametoa wito Kwa Wamiliki Wa Magari Hususani Mabasi Na Malori Kuhakikisha madereva Wote ambao waliowaajiri wanaanza wao kuwahakiki Kwanza ili kujiridhisha.
"Wamiliki Wa Vyombo Vya Usafiri nawataka wawe makini Katika Hili, Wahakikishe wanaowaajiri mpaka wanaowasimamia Kwa Sababu tuumegundua vile vile Kuna Uzembe unaofanyika.
"Ajali Ya Kongwa Uchunguzi Wa Awali unatupa ishara Kwamba waliokuwa wanaendesha Magari Yale Sio madereva, inaonekana Madereva ni Sehemu ya Majeruhi Wa hospitalini na Wamiliki waliwapa watu wasiokuwa na Vigezo" Amesema Masauni.
Aidha, Masauni Amesema Hatua Nyingine wanaichukua Juu ya Kupunguza Ajali za Barabarani wamepanga Kufanya Operation Kali ya Usiku na Mchana ambapo wataongeza Askari, watafanya Doria Za Usiku na Mchana Barabara Kuu Na kufuatilia mienendo ya Mabasi na Madereva.
Nae MKUU Wa JESHI La Polisi IGP Camilius Wambura, Amesema Kuhusu Suala la Rushwa Kwa Askari Wa Usalama Barabarani wanaendelea kuchukua Hatua Kali na Askari Yeyote atakayebainika kujihusisha na Rushwa atashughulikiwa ipasavyo.
No comments:
Post a Comment