MUSWAADA WA MAPITIO SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI KUWASILISHWA BUNGENI APRILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 7, 2023

MUSWAADA WA MAPITIO SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI KUWASILISHWA BUNGENI APRILI


Na Okuly Julius-Dodoma 

Muswaada wa mabadiliko ya Sheria za Huduma za Habari ya Mwaka 2016 unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Aprili 2023.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amesema muswada huo ulikuwa uwasilishwe katika Bunge la 12, Mkutano wa 10, Kikao cha Sita.

"Ni lazima tuwe na sheria ambayo kila mdau ana amani nayo, Serikali imesikiliza wadau wote imechukua mapendekezo ya wadau na kuyaweka kwenye muswada," amearifu Ndg. Msigwa.

Mabadiliko ya Sheria za Huduma za Habari 2016 ni miongoni mwa jitihada zinazochukuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.

No comments:

Post a Comment