![]() |
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la TaifalaUjenzi(NCC), Dk.Matiko Mturi akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Baraza hilo jijini Dodoma, Februari 13 mwaka huu mbele ya waandishi wa habari. |
BARAZA la Taifa la Ujenzi (NCC) imeendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi ambapo jumla ya mashauri sita yametolewa uamuzi huku mengine 31 yakiwa katika hatua mbalimbali za utatuzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Dkt.Matiko Mturi ameyasema hayo jijini Dodoma, Februari 13 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo.
Mtendaji mkuu huyo amesema kufuatia utekelezaji wa majukumu hayo wanayoshughulika nayo katika kipindi cha Julai 1,2022 hadi Januari 31, 2023 NCC imefanikiwa kutekeleza majukumu kadhaa ikiwemo kuandaa rasimu ya mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.
"Mipango ya utekelezaji kwa Februari 1, 2023 hadi Juni 30 ,2023 kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususan taasisi za umma zinazotekeleza miradi ya Miundombinu"amesema Dkt.Matiko.
NCC pia imefanikiwa kuandaa rasimu ya mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.
Pia amesema NCC umefanikiwa kuhamasisha uundwaji wa bodi za usajili na vyama vya wadau wa sekta ya ujenzi likiwa na lengo la kutoa fursa kwa wataalam katika sekta ya ujenzi kutekeleza kazi zao kwa kuongozwa na mifumo iliyowekwa na Serikali pamoja na kulinda taaluma katika sekta hiyo.
Mtendaji huyo amefafanua kuwa utatuzi wa migogoro hiyo ni sehemu ya majukumu yao kama baraza linaloshughulika na sekta ya ujenzi.
Pia amesema Baraza la Taifa la ujenzi linatoa huduma mbalimbali kwa wadau wa sekta ya ujenzi ikiwemo uratibu wa sekta,ushauri wa masuala yoyote yanayohusu sekta ya ujenzi,uratibu wa usuluhishi wa migogoro katika sekta ya ujenzi,
"Kutoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi,ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya ujenzi,utafiti,ukusanyaji,uchapishaji na usambazaji wa taarifa za sekta ya ujenzi na miongozo mbalimbali ya gharama za ujenzi nchini,"amesema Dkt Matiko.
No comments:
Post a Comment