PROF.MAKUBI AWAONGOZA WATUMISHI KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS LA UPANDAJI MITI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, February 12, 2023

PROF.MAKUBI AWAONGOZA WATUMISHI KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS LA UPANDAJI MITI.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof.Abel Makubi akishiriki zoezi la upandaji Miti katika eneo la Ofisi za Wizara ,upande wa Njedengwa Jijini Dodoma .


Na Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Pro.Abel Makubi amewaongoza Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Afya katika zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Wizara lililopo Njedengwa Jijini Dodoma .


Akizungumza katika zoezi hilo Prof.Makubi amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamisisha Jamii Kuhusu umuhimu wa kupanda miti na kutunza Mazingira

Deodatha Makani, Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu akishiriki katika zoezi la upandaji miti


" Sisi kama Wizara ya Afya tumeungana pamoja kuja hapa katika kiwanja chetu eneo la Njedengwa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya Kuja kufanya hili zoezi la upandaji wa miti hii ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuendeleza na kuboresha Mazingira yetu hapa Nchini kama ambavyo Mh.Makamu wa Rais amekuwa akisisitiza kwamba Taasisi zote za Serikali ni vizuri ziwe mbele kabisa katika kuhamasisha wananchi kupanda miti ili kuyalinda Mazingira yetu " Prof Makubi 

Aidha Prof Makubi amesema kuwa agizo hili limeanza kutekelezwa siku nyingi katika Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Afya ikiwa ni Pamoja na Hospital mbalimbali Nchini.


" Sisi kama Wizara tumeshafanya mazoezi haya ya upandaji miti na hili ni kama zoezi la tatu kuendelea kuhakikisha Mazingira yetu yote haya ambayo tunayamiliki sio tu Makao makuu lakini pia tuna Viwanja hapa Dodoma lazima tuhakikishe vinakuwa na Mazingira ambayo yamelindwa kwa kupanda miti "Prof Makubi 


  Kaimu Mkurugenzi Sehemu ya Elimu ya Afya Kwa Umma,Dkt.Tumaini Haonga akipanda  katika eneo ofisi za Wizara ya afya ,upande wa Njedengwa Jijini Dodoma .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya , Idara ya Kinga ,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt.Tumaini Haonga amemshukuru Katibu Mkuu pamoja na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara kwa kushiriki katika zoezi la upandaji miti kwenye Ofisi za Uchapaji Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

 " _Tunapozidi kuwa na Mazingira mazuri kwenye masuala ya Afya Kuna uhusiano wa Moja kwa moja kwenye kufanya kuleta Hewa safi ,mvua lakini pia kuwa na maeneo ya kupumzika" Dkt.Haonga 




Katika eneo hilo la Wizara ya Afya ambapo Kuna jengwa ofisi za Uchapaji pia kutakuwa na kumbi za mikutano ,Ofisi za studio ,kituo cha miito ya simu ambapo majengo hayo yatakapo kamilika watumishi wa Serikari watakuwa katika Mazingira ya ufanyaji kazi na kuwafanya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Pamoja na zoezi hilo upandaji la upandaji miti pia Katibu Mkuu Prof.Makubi amegawa miti kwa watumishi wa Wizara ya Afya ili kwenda kupanda katika maeneo ya makazi yao kwa lengo la kuboresha Mazingira na kustawisha Jiji la Dodoma.

Zoezi hilo limehusisha Viongozi mbalimbali waandamizi wa Wizara ya Afya akiwemo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Bi.Deordata Makani.

No comments:

Post a Comment